Hifadhi ya mazingira

mazoezi ya kulinda mazingira asilia kwa watu binafsi, mashirika na serikali

Hifadhi ya mazingira ni juhudi zinazofanywa na binadamu ili kuhakikisha ulimwengu anamoishi usiharibiwe na utendaji wake, bali uweze kuwafaa watu wa vizazi vijavyo.

Pundamilia, mbuga za Serengeti, Tanzania.

Tunatakiwa tutunze mazingira kwani tukiyachafua tutapata magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na mengine mengi.

Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka sisi wanadamu. Kwa mfano: miti, mito, maziwa, nyumba na kadhalika. Mazingira yanafaa kuwekwa safi wakati wote kwani yana faida kubwa katika maisha ya mwanadamu ingawaje katika dunia hii ya sasa watu wamekuwa wakiharibu mazingira yanayowazunguka. Mfano: watu wanakata miti ovyo, wanachafua vyanzo vya maji; uchafuzi huo unapelekea hata wanyama kukimbia makazi yao na kwenda kutafuta makazi mengine.

Pia kutokana na ukataji miti ovyo imepelekea ukosefu wa mvua, na hii imepelekea kuanguka kwa kilimo duniani na kusababisha njaa katika baadhi ya maeneo, hasa katika nchi za Asia.

Pia joto kuongezeka: kwa mfano huko India joto lilipanda juu sana hivyo kupelekea vifo.

Kwa hayo machache tunaona athari za uchafuzi wa mazingira; ni vyema tukajitahidi kuyatunza mazingira yetu ili kuweza kupata manufaa kutoka kwenye mazingira yetu wenyewe.

Ushauri kuhusu mazingira hariri

  • Usikate miti ovyo kwa maana hutasababisha ukame kwa kukosa mvua.
  • Usichome misitu.
  • Panda miti kwa wingi.
  • Usifuge mifugo mingi katika eneo dogo.
  • Panda mazao yanayoongeza rutuba kwenye ardhi.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hifadhi ya mazingira kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.