Historia ya Albania

Historia ya Albania inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Albania.

Historia ya kale hariri

Albania ilikaliwa na makabila mbalimbali ya Wailiriko, Wathraki na ya Wagiriki.

Katika karne ya 3 KK eneo lilitekwa na Dola la Roma na kufanywa sehemu ya majimbo ya Dalmatia, Masedonia na Iliriko.

Karne za Kati hariri

Mwaka 1190 ndani ya Dola la Roma Mashariki ulitokea ufalme mdogo wa Arbër kwa juhudi za archon Progon huko Krujë.

Mwishoni mwa karne ya 13 Charles wa Anjou aliwanyang'anya Wabizanti eneo hilo na kuanzisha Ufalme wa Albania kutoka Durrës hadi Butrint.

Katikati ya karne ya 15 nchi ilitekwa na Waosmani.

Historia ya kisasa hariri

Albania ya sasa ilitokea mwaka 1912, baada ya Waosmani kushindwa katika vita vya Balkani.

Ufalme wa Albania ulitekwa na Italia ya Benito Mussolini mwaka 1939 hadi 1943, ulipowekwa na Ujerumani wa Adolf Hitler chini yake.

Baada ya nchi hizo mbili kushindwa vitani, nchi ikaongozwa na Enver Hoxha ikijitenga zaidi na zaidi na dunia nzima.

Kati ya miaka 1945 na 1990 ilipotawaliwa na chama cha Kikomunisti Albania ilitangaza kuwa nchi ya kwanza ya kiatheisti na kupiga marufuku kila aina ya dini.

Kutokana na mapinduzi ya mwaka 1991 Jamhuri ya Kisoshalisti iliiachia nafasi jamhuri ya nne.

Kwa sasa Albania ni kati ya nchi maskini zaidi za Ulaya na wananchi wengi wamehama.

  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Albania kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.