Historia ya Amerika

Historia ya Amerika inasimulia matukio ya bara hilo lote (Amerika Kaskazini pamoja na Amerika ya Kati, Amerika Kusini na visiwa vya Karibi) tangu binadamu alipolifikia kutoka Asia.

Picha halisi ya Amerika kutoka angani mwaka 2001.
Ramani ya uenezi wa binadamu duniani.

Historia ya awali inaanza na kilele cha Enzi ya barafu, watu walipoweka kuingia Alaska kupitia nchi kavu. Baada ya hapo watu hao na wajukuu wao hawakuwa tena na uhusiano na wale wa "Dunia ya zamani" (Afrika, Asia na Ulaya) mpaka walipofikiwa na Wazungu kutoka Norway (karne ya 10) na Christopher Columbus mwaka 1492.

Hao wakazi wa kwanza walikuwa wawindaji na wachumaji. Wakifuata mawindo yao walifika taratibu hadi ncha ya kusini (Tierra del Fuego).

Polepole utamaduni wa baadhi ya makabila, ingawa kwa kuchelewa kuliko Dunia ya zamani, ulifikia hadhi ya ustaarabu, kama vile ule wa Norte Chico, Cahokia, Zapotec, Toltec, Olmec, Maya, Aztec, Purépecha, Chimor, Mixtec, Moche, Mississippi, Puebloan, Totonac, Teotihuacan, Huastec, Purépecha, Izapa, Mazatec, Muisca na Inca.

Safari za baharia Christopher Columbus kuanzia mwaka 1492, zilivuta hasa Hispania, Ureno na halafu Uingereza, Ufaransa na Uholanzi kujianzishia makoloni ili kunyonya maliasili nyingi za "Dunia mpya".

Kwa namna hiyo, mazingira ya Amerika yalibadilika kabisa mpaka zikatokea aina mpya za utamaduni na hatimaye mataifa mapya, hasa kutokana na mchanganyiko ya wenyeji (Waindio) na walowezi kutoka Ulaya, halafu pia watumwa kutoka Afrika.

Mgawanyiko mkuu uliojitokeza ni kati ya nchi za Kaskazini (inapotawala lugha ya Kiingereza na Ukristo wa madhehebu ya Uprotestanti: "Anglo-America") na zile za Kati na Kusini (zinapotawala lugha za Kihispania na Kireno na Kanisa Katoliki: "Latino-America").

Ukoloni huo ulidumu tangu mwanzo wa karne ya 16 hadi mwisho wa karne ya 18 na mwanzo wa ile ya 19, ambapo karibu makoloni yote yalijipatia uhuru.

Hasa nchi ya Marekani ilizidi kukua hata kushika nafasi ya kwanza duniani katikati ya karne ya 20.

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Boyer, Paul S. The Oxford Companion to United States History (2001) excerpt and text search; online at many libraries
  • Carnes, Mark C., and John A. Garraty. The American Nation: A History of the United States: AP Edition (2008)
  • Egerton, Douglas R. et al. The Atlantic World: A History, 1400–1888 (2007), college textbook; 530pp
  • Elliott, John H. Empires of the Atlantic World: Britain and Spain in America 1492–1830 (2007), 608pp excerpt and text search, advanced synthesis
  • Hardwick, Susan W., Fred M. Shelley, and Donald G. Holtgrieve. The Geography of North America: Environment, Political Economy, and Culture (2007)
  • Jacobs, Heidi Hayes, and Michal L. LeVasseur. World Studies: Latin America: Geography - History - Culture (2007)
  • Bruce E. Johansen, The Native Peoples of North America: A History (2006)
  • Keen, Benjamin, and Keith Haynes. A History of Latin America (2008)
  • Kennedy, David M., Lizabeth Cohen, and Thomas Bailey. The American Pageant (2 vol 2008), U.S. history
  • Marsh, James C., ed. The Canadian Encyclopedia (4 vol 1985) online edition Archived 27 Agosti 2008 at the Wayback Machine.
  • Morton, Desmond. A Short History of Canada 5th ed (2001)
  • Veblen, Thomas T. Kenneth R. Young, and Antony R. Orme. The Physical Geography of South America (2007)
  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Amerika kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.