Historia ya Latvia

Historia ya Latvia inahusu eneo la Ulaya ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Latvia.

Kwa muda mrefu Estonia ilikuwa chini ya Wajerumani, Wapolandi na Waswidi, halafu (1710) sehemu ya Dola la Urusi.

Katika miaka 1918-1940 ilikuwa jamhuri huru, halafu miaka 1940-1991 mwanachama wa Umoja wa Kisovyeti.

Baada ya umoja huo wa majimbo 15 kusambaratika, Latvia ilijitangaza tena nchi huru.

Latvia ilijiunga na Umoja wa Ulaya baada ya azimio la Halmashauri Kuu ya Ulaya ya tarehe 13 Desemba 2002 iliyokutana Kopenhagen.

Katika kura ya maoni ya tarehe 20 Septemba 2003 ni 66.9% za Walatvia wote waliokubali azimio hilo.

Latvia iliingia rasmi katika Umoja wa Ulaya tarehe 1 Mei 2004 pamoja na nchi nyingine 9 za Ulaya mashariki.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Latvia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.