Historia ya Morisi

Historia ya Morisi inahusu visiwa vya Bahari ya Hindi mkabala wa Afrika Mashariki ambavyo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Morisi.

Baada ya Waarabu na Wareno kuvumbua Morisi, wakazi wa kwanza (1638) walikuwa Waholanzi, lakini hawakuacha dalili isipokuwa majina ya mahali kwa sababu waliondoka mwaka 1710 baada ya kushindwa kiuchumi.

Wafaransa walitawala visiwa kati ya 1715 hadi 1810. Walianzisha miji na mashamba ya miwa. Nje ya walowezi, Wafaransa walipeleka pia watumwa kutoka bara la Afrika. Mwaka 1767 walikuwepo Wafaransa 3,163 pamoja na watumwa Waafrika 15,000, pia Wahindi 587.

Uingereza ulichukua utawala wa visiwa mwaka 1810 katika vita dhidi ya Napoleon.

Tangu siku zile Kiingereza kilikuwa lugha rasmi ya serikali, lakini wakazi waliendelea kutumia lahaja za Kifaransa.

Baada ya kuwapatia watumwa uhuru, Waingereza walileta Wahindi wengi, baadaye pia Wachina kama wafanyakazi kwenye mashamba ya sukari. Leo hii idadi kubwa ya wakazi ni wa asili ya Kihindi.

Nchi ilipata uhuru tarehe 12 Machi 1968, ikawa jamhuri tarehe hiyohiyo mwaka 1992.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Morisi kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.