Historia ya Ucheki

Historia ya Ucheki inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Ucheki.

Katika karne ya 7 nchi ilikuwa ufalme wa Moravia kuu.

Historia ya jamhuri ya Ucheki yenyewe si ndefu, tukiangalia tangu nchi hiyo kupokea uhuru kamili mwaka 1993 hadi leo.

Kabla ya hapo Ucheki ulikuwa umeungana na Slovakia kama Cheko-Slovakia (Chekoslovakia) ambayo tena ilikuwa kwanza chini ya utawala wa ufalme wa Austria-Hungaria katika karne ya 19 hadi mwanzo wa karne ya 20, yaani mpaka vita vikuu vya kwanza wakati ufalme uliposhindwa na kusambaratika.

Rais wa kwanza kuteuliwa kwa taifa hilo mpya ni Tomáš Garrigue Masaryk.

Wakati wa vita vikuu vya pili Wajerumani walichukua uongozi wa Chekoslovakia, lakini hawakudumu mno.

Kufikia mwisho wa vita hivyo USSR ilichukua unahodha na kuweka nchi hiyo katika sera ya Ukomunisti.

Wananchi walitawaliwa kwa nguvu halisi hadi mwaka 1989 wakati kulitokea mapinduzi ya amani na kupata uhuru halisi na demokrasia.

Mwaka 1993, nchi hiyo iligawanyika katika Ucheki na Slovakia kwa sababu ya kisiasa.

Mwaka 1999 nchi ya Ucheki ilijiunga na NATO.

Ucheki imekuwa mwanachama wa muungano ya Umoja wa Ulaya kuanzia mwaka 2004.

Ucheki ni maarufu katika dunia kwa usalama wake na inapendwa sana na mamilioni ya watalii ambao huizuru kila mwaka.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Ucheki kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.