Honshu (matamshi  Honshū ?) ni kisiwa kikubwa zaidi ya Japani.[1]

Ramani ikionyesha Honshu.

Japani ni Nchi za visiwa na Honshu ni kisiwa chake kikuu. Iko upande wa kusini wa Hokkaido iliyopo ng'ambo ya Mlangobahari wa Tsugaru, upande wa kaskazini wa Shikoku (ng'ambo ya Bahari ya ndani ya Seto, na upande wa Kyushu iliyopo ng'ambo ya mlangobahari wa Kanmon. Kwa ukubwa ni kisiwa cha saba duniani, na kwa idadi ya wakazi ni kisiwa cha pili, baada ya kisiwa cha Java.

Honshu ina urefu wa kilomita 1,300, upana wake hucheza baina ya km 50 hadi 230. Eneo lake ni kilomita za mraba 227,960. Mlima Fuji ambao ni volkeno na mlima mrefu wa Japan upo Honshu. Idadi ya wakazi ilikuwa mnamo milioni 104 katika mwaka 2017[2]. Miji mikubwa kama Tokyo inapatikana Honshu, pamoja na Yokohama, Kansai na Kyoto, Osaka na Kobe, pia Hiroshima, Akita na Nagoya.

Sawa na visiwa vingine vya Japani Honshu iko karibu na mstari ambako mabamba ya gandunia ya Pasifiki na ya Ufilipino huzama chini ya mabamba jirani na kusababisha kupanda juu kwa magma kutoka koti ya Dunia. Magma hiyo inajenga volkeno na mwendo wa mabamba ya gandunia husababisha mara kwa mara mitetemeko ya ardhi.

Honshu iliona mitetemeko mikubwa ya mara kwa mara; tetemeko la ardhi la mwaka 1923 liliua zaidi ya watu 100,000 katika mazingira ya Tokyo. Tetemeko la mwaka 2011 halikuua watu wengi vile kwa sababu sheria za ujenzi za Japani zilisababisha kujengwa kwa nyumba imara kuliko zamani. Lakini tetemeko hilo lilileta tsunami kadhaa zilizosababisha ajali ya nyuklia ya Fukushima.

Marejeo hariri

  1. Nussbaum, Louis-Frédéric. (2002). "Honshū" in Japan Encyclopedia, p. 351.
  2. Boquet, Yves (2017). The Philippine Archipelago. Springer. uk. 16. ISBN 9783319519265

Viungo vya Nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Japani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Honshu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.