Ieoh Ming Pei (*26 Aprili 1917 - 15 Mei 2019) ni msanifu majengo kutoka China anayeishi Marekani. Anapenda kutumia maumbo ya kijiometria akipendelea saruji, feleji, kioo na mwamba.

Piramidi ya Louvre (Paris)
Nyongeza ya Pei kwenye Makumbusho ya Berlin

Maisha hariri

Pei alizaliwa mjini Guangzhou (China). Alipokea masomo katika utamaduni wa Kichina lakini pia kwenye shule ya Kimarekani. 1935 akaenda Marekani kwa masomo ya usanifu majengo. Alisoma vitabu vya Le Corbusier na kuwa masaidizi wa Walter Gropius.

1942 alimwoa mama Mchina Ai-Ling Loon akazaa naye wavulana watatu na binti mmoja.

Kazi hariri

Baada ya kumaliza chuo kikuu aliamua kukaa MArekani kwa sababuy a vita ya wenyewe kwa wenyewe ya China ya miaka ya 1940 iliyoishia kwa ushindi wa Mao Tse Tung. Aliajiriwa na kampuni kubwa kama msanifu mkuu na 1960 aliunda kampni yake ya binafsi.

Alipata kazi nyingi akawa maarufu kwa uwezo wake wa kupanusha majengo ya kale akiunganisha mtindo wa kale na teknolojia ya kisasa. Kati ya majengo yake mashuhuri ni maktaba ya Kennedy mjini Boston na Piramidi ya Louvre mjini Paris.

Alijenga pia nyumba ya maghorofa kwa benki huko China.

1983 alipokea tuzo la usanifu la Pritzker.


Picha hariri

Viungo vya Njek hariri