Ikweta ya anga (en:celestial equator) ni mstari wa kudhaniwa kwenye anga unaotumiwa katika astronomia. Ni duara kubwa kwenye tufe la anga iliyopo juu ya ikweta ya Dunia. Ni kama pacha ya ikweta ya Dunia angani. [1]

Ikweta ya anga, Ekliptiki na Mhimili wa Dunia.

Kutokana na mwinamo wa mhimili wa mzunguko wa Dunia kuna pembe ya nyuzi 23.4 kati ya ikweta ya anga na bapa la ekliptiki.

Mtazamaji anayekaa kwenye ikweta ya Dunia (kwa mfano Nanyuki, Kenya) ikweta ya anga iko juu kabisa. Kwa mtazamaji kwenye ncha za Dunia ikweta ya anga ni sawa na upeo wa macho.

Upande wa kusini wa ikweta ya anga huitwa angakusi, upande wa kaskazini angakaskazi. Mtazamaji aliye kwenye ncha za Dunia anaona tu ama nyota za angakusi ama zile za angakaskazi. Mtazamaji aliyeko kwenye ikweta ataona nyota za pande zote mbili.

Tanbihi

  1. "Celestial Equator". Iliwekwa mnamo 5 August 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ikweta ya anga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.