Ishara ni kitu kinachobainika kwa macho kinachodokeza kutokea kwa jambo fulani (dalili).

Ishara ya ukaribisho ya barabarani nchini Colombia

Ishara zipo za aina nyingi: kuna ishara za barabarani ambazo huwaongoza madereva na wote wanaotumia barabara pindi wawapo barabarani.

Pia kuna ishara wanazotumia wanadamu kuwasiliana. Ishara hizo nazo zipo tofautitofauti kwani kuna ishara wanazotumia marafiki walioshibana kwa kuwasiliana, kama vile kutumia vidole au kichwa lakini pia kuna lugha ya ishara ambayo hutumiwa na walemavu wa masikio au wenye usikivu hafifu wakati wa kuwasiliana ana kwa ana au kupitia runinga.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ishara kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.