Iwambi ni kata ya Mbeya Mjini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Iko kati ya Iyunga na Mbalizi kando ya barabara kuu inayoelekea Vwawa na Zambia.

Kata ya Iwambi
Kata ya Iwambi is located in Tanzania
Kata ya Iwambi
Kata ya Iwambi

Mahali pa Iwambi katika Tanzania

Majiranukta: 8°53′24″S 33°25′48″E / 8.89000°S 33.43000°E / -8.89000; 33.43000
Nchi Tanzania
Mkoa Mbeya
Wilaya Mbeya Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 19,798

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 19,798 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,387 [2] walioishi humo.

Msimbo wa posta ni 53115.

Iwambi ni kata ambayo kihistoria walipatikana kabila la Wasafwa ambao waliongea lugha yao ya Kisafwa pia waliongozwa na mwene Mpoli ambaye alifariki mwaka 2005 na alizikwa ndani ya Iwambi katika mtaa wa Ivwanga.

Kati ya wenyeji mashuhuri wa Iwambi ni John Butler Walden (1939 – 2002) aliyekuwa kiongozi mmojawapo wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakati wa Vita vya Kagera dhidi ya Uganda. Kaburi lake linapatikana Iwambi.

Katika kata ya Iwambi kuna shule mbili za msingi ambazo ni shule ya msingi Iwambi ipo katika mtaa wa Mayombo na shule ya msingi Iyunga ipo katika mtaa wa Isoko. Pia KUna shule moja ya sekondari Iwambi iliyoanzishwa mwaka 2006 chini ya uongozi wa rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Mbeya - Mbeya MC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-14. 
  Kata za Jiji la Mbeya - Tanzania  

ForestGhanaIdudaIganjoIganzoIgawiloIlemiIlombaIsangaIsyesyeItaganoItendeIteziItijiIwambiIyelaIyungaIziwaKalobeMaangaMabatiniMaendeleoMajengoMbalizi RoadMwakibeteMwasangaMwasenkwaNondeNsalagaNsohoNzovweRuandaSindeSisimbaTembelaUyole


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Iwambi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.