Jack Steinberger (amezaliwa 15 Mei 1921) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Alizaliwa Ujerumani lakini akapahama wakati wa utoto wake kwa sababu ya utawala wa Wanazi. Hasa alichunguza sehemu za atomu na kujulikana kwa kugundua neutrino ya muon. Mwaka wa 1988, pamoja na Melvin Schwartz na Leon Lederman alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

Jack Steinberger
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jack Steinberger kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.