Jay-Z

Rapa wa Marekani na mfanya Biashara kutoka New York City


Shawn Corey Carter (amezaliwa tar. 4 Desemba 1969[1]) ni msanii wa hip hop na mfanyabiashara kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Jay-Z. Huyu ni Ofisa Mkuu wa zamani wa Def Jam Recordings[2] na Roc-A-Fella Records.

Jay-Z
Jay-Z, mnamo 2011
Jay-Z, mnamo 2011
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Shawn Corey Carter
Amezaliwa 4 Desemba 1969 (1969-12-04) (umri 54)
Brooklyn, New York, Marekani
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Rapa, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi
Ala Sauti
Miaka ya kazi 1986 – hadi
Studio Roc Nation/Atlantic Records
Ame/Wameshirikiana na Jaz-O, Memphis Bleek, Beanie Sigel, Amil, Beyoncé, Linkin Park, Kanye West, R. Kelly, T.I., UGK, Lil Wayne, Freeway, The Notorious B.I.G., Nas, Sean Combs, Foxy Brown, Pharrell, Coldplay, Eminem
Tovuti www.jay-z.com

Pia ni mmoja kati ya wanaomiliki klabu ya The 40/40 Club na New Jersey Nets. Huyu ni mmoja kati ya wasanii na mjasiriamali wa hip hop wa Marekani wenye mafanikio makubwa kabisa,[3] kwa kuuza nakala zaidi ya milioni 26 nchini Marekani na kupokea Tuzo za Grammy kadhaa kwa kazi zake za kimuziki.[4]

Pamoja na kuwa na mafanikio yake makubwa ya kimuziki, Jay-Z anafahamika zaidi kwa kujihusisha na masuala ya ugomvi na baadhi ya wasanii wengine wa soko zima la rap, moiongoni mwa ugomvi mkubwa uliokuwa unajulikana na watu wengi duniani ni ule wa yeye na rapa mwenziwe wa mjini New York Bw. Nas, ambao ulikuja kusuluishwa mnamo mwaka wa 2005.

Jay-Z alitoa albamu yake ya kwanza iliitwa Reasonable Doubt, ilipewa sifa na Rolling Stone kama albamu #248 ikiwa kama "Albamu Kali 500 za Karne". Albamu yake iliyompa sifa zaidi ni ile ya The Blueprint, iliandikwa kwa siku mbili tu, basi.[5]

Baada ya kujitangaza kwamba anastaafu muziki mnamo mwaka wa 2003, alirejea tena kazini mwishoni mwa mwaka wa 2006 na albamu yake ya Kingdom Come, ambayo iliuza kopi 680,000 katika wiki ya kwanza, na kuifanya iwe albamu ya Jay-Z iliofanya mauzo ya juu katika kipindi cha wiki ya kwanza.[6]

MTV wamemwita kama msanii wa kwanza katika orodha ya Ma-MC wao wa karne. Mnamo mwezi wa Aprili 2008, Jay-Z ameripotiwa kwenye verge kwamba ameingia ubia na Live Nation kwa kaisi cha Dola za Kimarekani zipatazo milioni 150—ambapo ni miongoni mwa mikataba mikubwa sana na ghari kwa wasanii wambo waliowahi kuungana nao.[7]

Carter amemwoa Bi. Beyoncé Knowles mnamo tar. 4 Aprili 2008.[8]

Wasifu hariri

Maisha ya awali hariri

Mtu huyu amekuwa akihusishwa na nadharia mbalimbali ambazo zinaamini kuwa jay z amekuwa akifa na kuzaliwa upya hii inathibitishwa na picha take aliyppiga mnamo mwaka 1929 huko jijini network akiwa kijana amekuwa ukiulizwa na kusema kuwa yeye ni "young forever" yani mdogo milele

Discografia hariri

Solo albamu
Albamu za Kolabo
Kompilesheni albamu
  • Jay-Z: Unplugged (2001)
  • Chapter One: Greatest Hits (2002)
  • The Blueprint 2.1 (2003)
  • Bring It On: The Best of Jay-Z (2003)
  • Greatest Hits (2006)

Tuzo hariri

Filmografia hariri

Filamu Mwaka
Streets Is Watching 1998
Backstage 2000
State Property 2002
Paper Soldiers 2002
Fade to Black 2004
Diary of Jay-Z: Water for Life 2006

Marejeo hariri

  1. Jay-Z. Internet Movie Database. Imeingizwa tar. 23 Oktoba 2008.
  2. "Pitchfork: Jay-Z Leaves Def Jam Presidency". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-07-24. Iliwekwa mnamo 2007-07-24. 
  3. The Greatest MCs of All Time MTV. Retrieved on 2006-12-26
  4. "RIAA - Gold & Platinum - August 08, 2008". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-07-01. Iliwekwa mnamo 2009-06-13. 
  5. Recounted by Jay-Z on the documentary Collision Course DVD. Collision Course. Jay-Z and Linkin Park. Roc-A-Fella/Warner Bros./Machine Shop Recordings. 2004.
  6. Jay-Z Reclaims His 'Kingdom' With No. 1 Debut Archived 27 Oktoba 2012 at the Wayback Machine.. Billboard.com. Retrieved on 29 Novemba 2006.
  7. Leeds, Jeff. "In Rapper’s Deal, a New Model for Music Business", New York Times, 2008-04-03. Retrieved on 2008-04-03. 
  8. Source: Beyoncé and Jay-Z Are Married

Viungo vya Nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: