Jay Moe

mwanamuziki wa Tanzania

Juma Mohamed Mchopanga (maarufu kwa jina lake la kisanii Jay Moe; amezaliwa 27 Novemba 1978 kwenye hospital ya Hindu Mandal katika jiji la Dar es salaam. ni mwanamuziki wa Rap, mtunzi wa nyimbo, mwigizaji, mpishi, mwanaharati na youtuber kutoka Tanzania mmoja kati ya msanii maarufu mali ya watu wa makonde. Ni lejendari na mashuhuri wa muziki wa "Bongo Flava & Bongo Rap", ambayo inachanganya vionjo vya muziki wa Hip Hop wa Marekani na ladha za asili za Kitanzania. Anasifiwa kwa utunzi mzuri sa mashairi ya kiswahili yanayohusu masuala ya kijamii ya Tanzania kama vile VVU/UKIMWI, madawa ya kulevya, elimu, umasikini, Maendeleo vijijini na masuala mengine ya kijamii. [1]

Jay Moe
Jay Moe
Jay Moe
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Juma Mohamed Mchopanga
Pia anajulikana kama Moe Tekniks
Moe Flava
Superman
Mawazo
Mr. Famous
Amezaliwa 27 Novemba 1978 (1978-11-27) (umri 45)
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Mwimbaji/Mtunzi/Mtayarishaji
Miaka ya kazi 1998-hadi leo
Ame/Wameshirikiana na TID
Mwana F.a
Ngwair
MIMS
King Kaka
Chidi Benz
JCB
Lord Eyez

Maisha ya Muziki hariri

Alianza kurap mwaka wa 1998 akiwa mwanachama wa kundi la WATEULE, maarufu kwa vibao vyao "Watu Kibao", "Tumerudi Tena", na "Bado Yuko Vile vile".

Katika kipindi chake cha solo iliyoanza mwaka wa 2001, ametoa vibao kadhaa, vikiwemo "Bishoo", "Kama unataka demu", "Mvua na jua".  Nyimbo nyingine alizotoa Jay Moe ni pamoja na "Story 3" na "Kimya kimya" feat. Mangwair. Kama ilivyo kwa Profesa Jay, Fid Q na Mwana F.a, yeye ni MC mkongwe wa Tanzania, ambaye amesalia kuwa baadhi ya wanamuziki maarufu wa hip hop nchini Tanzania, licha ya kufurika kwa wazabuni wengi wapya.  Katika mojawapo ya nyimbo zake amewahi kulinganisha kati ya mvua na jua bora nini, wimbo huo wenye chorus inayosema maneno "Kati ya mvua na jua bora nini?" kati ya nyimbo zenye muda mrefu ambazo bado kila kukicha zinapigwa maredio na sehemu nyingine za starehe.

Albamu yake ya kwanza,"Ulimwengu ndio mama," ilipata kutambuliwa papo hapo ambapo Jay Moe aliweza kufanya ziara nchi nzima, kupata nafasi ya kuigiza kwenye filamu ya girlfriend, filamu inayochukuliwa na wengi kama mwanzo wa kiwanda cha filamu za tanzania.

Nyimbo za Jay Moe ni pamoja na Never be me (aliomshirikisha MIMS kutoka Marekani), Maisha Ya Boarding aliomshirikisha Dully Sykes, Narudi Shule aliomshirikisha Mwana FA, Safari njema aliomshirikisha Dudu Baya na Complex), Mshamba akimshirikisha Juma Nature. pia ameshirikishwa na Ferooz kwenye wimbo wa Jirushe, TID Zeze na Girlfriend; Mwana FA Ingekuwa Vipi Profesa Jay Tathmini na wimbo wa Jajimental akishirikiana na Young Dee, Machizi Mmeniroga akishirikiana na Stamina.

Albamu hariri

  • Ulimwengu Ndio Mama 2002
  • Mawazo Ya Jay Moe 2004

Tuzo hariri

  • 2011 Tanzania Music Awards (Kilimanjaro Music Awards)- Best Hip Hop Song/ Best Callabo ("Ukiskia Paa")

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jay Moe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Marejeo hariri

  1. Jay Moe (en). Music In Africa (2014-07-23). Iliwekwa mnamo 2024-01-13.