Jibuti (Kifaransa: Djibouti; Kiarabu: جيبوتي), kirasmi Jamhuri ya Jibuti, ni nchi ndogo ya Afrika ya Mashariki kwenye Pembe la Afrika.

Jamhuri ya Jibuti
جمهورية جيبوتي (Kiarabu)
République de Djibouti (Kifaransa)
Jamhuuriyadda Jabuuti (Kisomali)
Gabuutih Ummuuno (Kiafar)
Kaulimbiu ya taifa:
اتحاد، مساواة، سلام (Kiarabu)
Unité, Égalité, Paix (Kifaransa)
Midnimo, Sinnaan, Nabad (Kisomali)
Inkittiino, Qeedala, Wagari (Kiafar)
"Umoja, Usawa, Amani"
Wimbo wa taifa: Jibuti
Mahali pa Jibuti
Mahali pa Jibuti
Ramani ya Jibuti
Ramani ya Jibuti
Mji mkuu
na mkubwa nchini
Jibuti
11°36′ N 43°10′ E
Lugha rasmi
Lugha za taifa
Makabila (asilimia)60 Wasomali
35 Waafar
5 Waarabu
SerikaliJamhuri yenye mdikteta
 • RaisIsmaïl Omar Guelleh
Eneo
 • Eneo la jumlakm2 23 200[1]
Idadi ya watu
 • Kadirio la 2023976 143[1]
Pato la taifaKadirio la 2023
 • JumlaOngezeko USD bilioni 3.873[2]
 • Kwa kila mtuOngezeko USD 3 761[2]
Pato halisi la taifaKadirio la 2023
 • JumlaOngezeko USD bilioni 7.193[2]
 • Kwa kila mtuOngezeko USD 6 985[2]
SarafuFaranga ya Jibuti
Majira ya saaUTC+3
(Afrika Mashariki)
Upande wa magariKulia
Msimbo wa simu+253
Msimbo wa ISO 3166DJ
Jina la kikoa.dj

Imepakana na Eritrea, Ethiopia na Somalia upande wa bara. Kuna pwani ya Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden. Ng'ambo ya bahari iko nchi ya Yemen katika umbali wa km 20 pekee.

Jina la nchi linatokana na lile la mji mkuu, Jibuti.

Jiografia hariri

Hali ya nchi inalingana kwa karibu na ile ya mataifa mengine katika Mashariki mwa Afrika, Jibuti ilipo, ikipakana na Ghuba ya Aden na Bahari ya Shamu, katikati ya Eritrea, Ethiopia na Somalia.

Eneo hariri

Kwa km 13 Jibuti inapakana na Eritrea, huku kukiwa na urefu wa kilomita 337 za mpaka kati ya Jibuti na Ethiopia, na mpaka wa km 58 na Somalia. Kwa jumla ina mpaka wa km 506. Pia ina pwani ya urefu wa km 314.

Jibuti inakaa kaika eneo la kufana, ikiwa karibu na leni zenye shughuli nyingi zaidi duniani la meli na pia karibu na mahali pa uchimbaji mafuta nchini Saudia.

Jibuti pia ni kituo cha reli ya Ethiopia-Jibuti.

Hali ya hewa hariri

Hali yake ya hewa ni ya joto kiasi, na pia haina mvua (ni jangwa).

Miinuko hariri

Milima iliyopo katikati ya nchi hugawa tambarare za pwani kutoka plateau. Eneo la chini zaidi ni Ziwa Assal mita 155 chini ya usawa wa bahari na la juu zaidi ni volikano Moussa Ali yenye kimo cha mita 2028. Hakuna shamba la ukulima, unyunyizaji maji, mimea iliyojimeza huko (msitu upo tu katika milima ya Goda, hasa mbuga ya Day Forest). Takribani asilimia 9 ya nchi ni malisho yeliyojimeza (1993 mashariki). Kwa hiyo Jibuti inahesabiwa kuwa sehemu ya nyasi ya Ethiopia, isipokuwa kijisehemu kinachopakana na Bahari ya Shamu ambacho ni baadhi ya Jangwa la Pwani ya Eritrea ambayo inajulikana kuwa njia nzuri ya uhamiaji wa ndege ambao wanaweza kuwindwa[3].

Mazingira hariri

Matukio ya kimaumbile ni pamoja na Matetemeko ya ardhi, kiangazi, mawimbi kutoka Bahari ya Hindi ambayo husababisha mafuriko na mvua kubwa. Malighafi ni pamoja na umeme kutoka ardhini (geothermal energy). Eneo hili limekumbwa na uhaba wa maji salama ya kunywa na pia kugeuka kwa eneo hilo kuwa jangwa.

Jibuti ni mwanachama wa makubaliano ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, ueneaji wa jangwa, viumbehai vilivyo hatarini, sheria ya bahari, kulinda ukanda wa ozoni na uharibifu wa mazingira na meli.

Historia hariri

Nchi ilikuwa koloni la Ufaransa kwa jina la Somalia ya Kifaransa, halafu (1967) Eneo la Kifaransa la Waafar na la Waisa, kutokana na majina ya makabila mawili makubwa zaidi ya eneo hilo.

Sababu ya kuanzishwa kwa koloni ilikuwa nia ya Ufaransa ya kuwa na bandari ya mji wa Jibuti karibu na Bab el Mandeb inayotawala mawasiliano kati ya Bahari Hindi na Bahari ya Shamu kuelekea Mfereji wa Suez.

Nchi ilipata uhuru tarehe 27 Juni 1977.

Hadi leo umuhimu na uchumi wake unategemea bandari, ambapo zinapitia asilimia 95 za bidhaa zinazoingizwa Ethiopia. Nchi hiyo imeunganishwa na Jibuti kwa reli, moja ya zamani, na nyingine mpya iliyokamilika mwaka 2016.

Watu hariri

Siku hizi wakazi wengi (60%) ni Wasomali, hasa wa kabila la Waisa, halafu Waafar (35%). Asilimia 5 zilizobaki ni Waarabu, Waethiopia na Wazungu (hasa Wafaransa na Waitalia).

Lugha rasmi ni Kifaransa na Kiarabu. Kisomali na Kiafar ni lugha za taifa.

 
Ismaaciil Cumar Geelle.

Upande wa dini, Uislamu unafuatwa na 94% za wakazi na ndio dini rasmi pekee. Asilimia 6 wanafuata Ukristo katika madhehebu mbalimbali, hasa Waorthodoksi wa Mashariki kutoka Ethiopia (3.2%), halafu Wakatoliki (1.4%) na Waprotestanti (chini ya 1%).

Tazama pia hariri

 
Bunge.

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 "Djibouti". The World Factbook (kwa Kiingereza) (toleo la 2024). Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo 30 March 2024.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "World Economic Outlook Database, October 2023 Edition. (Djibouti)". IMF.org. International Monetary Fund. 10 October 2023. Iliwekwa mnamo 20 October 2023.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. http://www.worldwildlife.org/wildworld/profiles/terrestrial/at/at1304_full.html

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla
Mengineyo


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jibuti kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.