Jongoobahari
Mbura kahawia (Actinopyga echinites)
Mbura kahawia (Actinopyga echinites)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
Faila ya juu: Deuterostoma
Faila: Echinodermata
Nusufaila: Echinozoa
Ngeli: Holothuroidea
Blainville, 1834
Ngazi za chini

Nusungeli na oda:

Majongoobahari (pia hujulikana kama jongoo la pwani, kojojo, kojokojo, babaje, kiazi, matiti) ni wanyama wa baharini kwenye ngeli Holothuroidea katika faila Echinodermata (wanyama ngozi-miiba). Jongoobahari wana ngozi ngumu na mwili mrefu wenye via vya uzazi moja iliyo na matawi. Wanyama hawa wanapatikana kwenye sakafu za bahari duniani kote, wakiwa wamegawanyika kwenye spishi zipatazo 1,717. [1]Nyingi ya hizi spishi zinapatikana eneo la Asia-Pasifiki.[2]

Majongoobahari yana mchango muhimu kwenye mfumo wa ekolojia wa bahari kwa kusaidia kuzungusha virutubishi na kuvunjavunja mabaki na uchafu wa kioganiki wa baharini hivyo kuruhusu bakteria kuendelea na mchakato wa kuvunjavunja. Majongoobahari hukusanywa kwa ajili ya chakula japo baadhi ya spishi zinalimwa kwa kilimo cha majini. Majongoobahari yanayookotwa yanajulikana kwa majina mengi yakiwemo trepang, namako, bêche-de-mer au balate.[2]

Kama walivyo wanyama ngozi-miiba wote, majongoo-bahari pia wana mjengo wa mwili wa ndani (kiunzi ndani) chini ya ngozi ambao mara nyingi unakua kwa muundo wa vifupa vidogo vidogo vya kihadubini vinavyounganishwa na tishu unganishi. Kwenye spishi nyingine mjengo wa mwili unakua kama visahani vyembamba vinavyofunika mwili. Spishi za kipelagia kama Pelagothuria natatrix (oda Elasipodida, familia Pelagothuriidae) hazina mjengo wa mwili.[3]

Kwa lugha ya Kiingereza jongoobahari huitwa 'sea cucumbers', ikimaanisha matango bahari kutokana na kufanana kwao na matunda ya mtango.

Jongoobahari wa Afrika Mashariki hariri

Picha hariri

Mwainisho wa kisayansi hariri

Mwainisho wa kisayansi kadiri ya World Register of Marine Species:

Matumizi hariri

Chakula hariri

Jongoobahari wamekua wakitumika kama chakula kwa miaka mingi, soko kubwa likiwa kusini mwa China. Baadhi ya spishi ambazo huliwa sana ni:

Dawa hariri

Jongoobahari husemekana wanatumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo maumivu ya viungo na kasna japo hakuna ushahidi wa kisayansi kuthibitisha hayo. Utafiti unaendelea ili kujua labda baadhi ya kompaundi zilizopo kwenye jongoobahari zinaweza kua na tabia za kuzuia magonjwa kama kansa.

Tanbihi hariri

  1. Paulay, G. (2014). Holothuroidea. World Register of Marine Species.
  2. 2.0 2.1 Du H.; Bao Z.; Hou R.; Wang S.; Su H. (2012). "Transcriptome Sequencing and Characterization for the Sea Cucumber Apostichopus japonicus (Selenka, 1867)". PLOS ONE 7 (3): e33311. Bibcode:2012PLoSO...733311D. PMC 3299772. PMID 22428017. doi:10.1371/journal.pone.0033311.  Unknown parameter |doi-access= ignored (help)
  3. Reich, Mike (30–31 January 2006). Lefebvre, B.; David, B.; Nardin, E. et al., eds. "Cambrian holothurians? – The early fossil record and evolution of Holothuroidea". Journées Georges Ubaghs: 36–37. Archived from the original on February 25, 2009.  Unknown parameter |url-status= ignored (help);
  4. Mmbaga T.K. and Mgaya Y. D (2004). Sea cucumber fishery in Tanzania. Advances in sea cucumber aquaculture and management. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-02-17. Iliwekwa mnamo 2021-10-31.