Juliani wa Sora (alifariki Sora, Lazio, Italia, 161 hivi) alikuwa Mkristo aliyeuawa kwa kukatwa kichwa wakati wa dhuluma ya kaisari Antoninus Pius dhidi ya imani hiyo kwa kuwa alihubiri Injili akitokea Dalmatia (leo nchini Kroatia) na kuelekea Campania[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Wa kwanza wanaadhimisha sikukuu yake tarehe 27 Januari[2], wa pili tarehe 11 Agosti[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. St. Julian of Sora Catholic Online
  2. Martyrologium Romanum
  3. "The Holy Martyr Julian. Commemorated July 28 (Civil Date: August 11 )". www.orthodox.net (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2017-03-01. 
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.