Kaisari Justiniani II (668/669 - 4 Novemba 711) alitawala Dola la Roma Mashariki kuanzia mwaka 685 hadi 695, tena kutoka 705 hadi 711, alipouawa kwa kiburi na ukatili wake.

Justiniani II katika mozaiki huko Ravenna, Italia.

Alijitahidi kurudisha Dola la Roma katika hadhi yake ya zamani.

Katika historia ya Kanisa anakumbukwa kwa kuendesha mtaguso wa tano-sita katika ikulu yake.

Tangu kale Waorthodoksi wanamheshimu kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Agosti[1][2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Vyanzo hariri

Vyanzo vikuu hariri

Vinginevyo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: