Kairuan (pia Kairouan au Al Qayrawān) ni mji mkuu wa Wilaya ya Kairouan nchini Tunisia. Mji huo umepokewa na UNESCO katika orodha ya Urithi wa Dunia.

Kairouan

Mji ulianzishwa na Wamuawiya baada ya uenezi wa Waarabu Waislamu mnamo mwaka 670. [1] Katika kipindi cha Khalifa Mu'awiya (661-680) ulikuwa kituo muhimu cha usomi wa Kiislamu wa Kisunni na ujifunzaji wa Qur'ani [2] na hivyo kuvutia Waislamu wengi kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu. Hadhi yake ilipitwa tu na Makka, Madina na Yerusalemu. Msikiti mtakatifu wa Uqba uko katika mji huo. [3]

Mnamo 2014, jiji lilikuwa na wakazi wapatao 187,000[4]..

Mskiti Kuu ya Kairouan

Picha za Kairuan hariri

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. Nagendra Kr Singh, International encyclopaedia of Islamic dynasties. Anmol Publications PVT. LTD. 2002. page 1006
  2. Luscombe, David; Riley-Smith, Jonathan, wahariri (2004). The New Cambridge Medieval History, Volume 2; Volume 4. Cambridge University Press. uk. 696. ISBN 9780521414111. 
  3. Hutchinson Encyclopedia 1996 Edition. Helicon Publishing Ltd, Oxford. 1996. uk. 572. ISBN 1-85986-107-5. 
  4. Recensement de 2014 (Institut national de la statistique) Archived 2014-10-29 at the Wayback Machine

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Tunisia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kairuan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.