Kalimantan (inajulikana pia kwa jina la Borneo ya Indonesia) ni sehemu kubwa ya kisiwa cha Borneo iliyopo Indonesia.[1] Sehemu hii ni asilimia 73 za eneo lote la kisiwa hicho. Sehemu nyingine zisizo za Indonesia ni Brunei na Malaysia ya Mashariki.

Ramani ya Kalimantan na sehemu zake

Etimolojia hariri

Jina la Kalimantan (pia Klemantan) linatokana na lugha ya {{Kisanskrit]]: Kalamanthana ikimaanisha kisiwa chenye hali ya hewa joto sana. Linafanywa na maneno mawili: kal(a) (wakati. majira) na manthan(a) (moto sana, ya kuchoma). [2]

Eneo hariri

Sehemu hii ya Indonesia ina asilimia 73 (km² 544,150 [3]) za kisiwa chote cha Borneo na 69.5% (watu 13,772,543 wakati wa sensa ya 2010) za wakazi wa kisiwa hiki. Sehemu zisizo za Kiindonesia ni Brunei (wakazi 400,000) na Malaysia ya Mashariki (wakazi 5,625,000) inayokumlisha majimbo ya Sabah, Sarawak na eneo la Labuan.

Utawala hariri

Kalimantan ina mikoa 5 :

Mikoa ya Kalimantan
Mkoa Eneo(km2) Wakazi (2005C) Wakazi (2010C) Wakazi (2015C prelim) Watu/km2 Makao makuu ya mkoa Mji mkubwa
West Kalimantan
(Kalimantan Barat)
147,307.00 4,042,817 4,393,239 4,783,209 32.5 Pontianak Pontianak
Central Kalimantan
(Kalimantan Tengah)
153,564.50 1,913,026 2,202,599 2,490,178 16.2 Palangkaraya Palangkaraya
South Kalimantan
(Kalimantan Selatan)
38,744.23 3,271,413 3,626,119 3,984,315 102.8 Banjarmasin Banjarmasin
East Kalimantan
(Kalimantan Timur)
129,067 2,840,874 3,550,586 3,422,676* 26.5 Samarinda Samarinda
North Kalimantan
(Kalimantan Utara)
71,176.72 473,424 524,526 639,639 8.5 Tanjung Selor Tarakan
Total 544,150.07 12,541,554 14,297,069 15,320,017 28 - Banjarmasin

Marejeo hariri

  1. Kalimantan. Britannica. Iliwekwa mnamo 2008-02-26.
  2. Central Kalimantan Province. archipelago fastfact. Iliwekwa mnamo 13 October 2014.
  3. Indonesia General Info. Geohive.com. Iliwekwa mnamo 2009-08-11.