Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia

Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia (kwa Kiamhara የኢትዮጵያ:ኦርቶዶክስ:ተዋሕዶ:ቤተ:ክርስቲያን, Yäityop'ya ortodoks täwahedo bétäkrestyan) ni madhehebu ya dini ya Ukristo iliyotawala watu wa jamii ya Waamhara kwa karne kadhaa hadi sasa.

Kanisa kuu la Utatu mtakatifu, Addis Ababa.

Wakristo hao wanaotaka kuzingatia imani sahihi ni sehemu muhimu katika utamaduni wa Ethiopia na Eritrea[1].

Kwa sasa ni kubwa zaidi duniani kuliko mengine yote ya jamii ya Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki, likiwa na waumini milioni 45-50.[2] wengi wao wakiishi nchini Ethiopia,[3] lakini pia Mashariki ya Kati, Ulaya na Amerika.

Historia hariri

 
Padri wa Kiethiopia akionyesha misalaba kwa ajili ya maandamano ya ibada.

Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia linaendeleza ushirika na Kanisa la Misri tangu lilipoanzishwa na mtakatifu Frumensyo aliyetumwa na mtakatifu Atanasi, Patriarki wa Aleksandria katikati ya karne ya 4 BK.

Hata hivyo mwaka 1959 lilikubaliwa liwe na Patriarki wake mwenyeji na kujiongoza.

Kwa jumla majimbo ni 44 na maaskofu 60.

Kalenda hariri

Kufuatana na mapokeo ya huko Misri, Epifania na Pasaka ni sikukuu muhimu sana, na husherehekewa kwa kufanya mambo kama vile kufunga kula na kucheza.

Pia kuna siku kadhaa katika mwaka ambapo ni mboga za majani pekee na samaki ndio huruhisiwa kuliwa.

Desturi hariri

Ndoa huweza kuanzishwa au kupangwa wakati mwanamume ana umri wa miaka kumi na..., au ishirini na... Kiutamaduni, wasichana wanaruhusiwa kuolewa wakiwa na umri wa miaka 14 hadi 18, lakini katika karne ya 20, mambo yamebadilika, hivyo sasa umri mdogo kuliko wote wa kuolewa ni miaka 18, na suala hili linasimamiwa na serikali. Ndoa za kiserikali ni nyingi japo pia, wapo watu wanaofunga ndoa katika makani mbalimbali. Na baada ya kufunga ndoa kanisani, suala la talaka halipo na haliwezekani. Kila familia hufanya sherehe ya ndoa baada ya harusi.

Tangu kuzaliwa, padri hutembelea familia kwa ajili ya kumbariki mtoto, na pia kutahiri mtoto kama ni wa kiume. Mama wa mtoto, hutakiwa kukaa ndani kwa siku 40 baada ya kujifungua kama mtoto ni wa kiume na kukaa ndani kwa siku 80 kwa mtoto ni wa kike kabla ya kwenda kanisani kwa ajili ya ubatizo.

Sanaa hariri

 
Picha takatifu ya Kiethiopia inayowaonyesha Yesu msulubiwa, Bikira Maria na mtakatifu Joji.

Sanaa ya nchini Ethiopia kwa ujumla imeegamia katika masuala ya dini na michoro ya dini.

Mmoja kati ya michoro mizuri zaidi ya vitu au watu wenye macho makubwa na mara nyingi huwa ni watu wanaohusiana na Biblia.

Tanbihi hariri

  1. FDRE States: Basic Information - Amhara Archived 10 Machi 2007 at the Wayback Machine., Population (accessed 26 Machi 2006)
  2. Ethiopia: Orthodox Head Urges Churches to Work for Better World. Iliwekwa mnamo 2006-09-13.
  3. Berhanu Abegaz, "Ethiopia: A Model Nation of Minorities" (accessed 6 April 2006)

Marejeo hariri

  • Archbishop Yesehaq. 1997. The Ethiopian Tewahedo Church: an Integrally African Church. Winston-Derek Publishers.
  • Mikre-Sellassie Gebre-Amanuel. 1993. “The Bible and Its Canon in the Ethiopian Orthodox Church.” The Bible Translator 44/1:111-123.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.