Katerina Labouré (Fain-les-Moutiers, Côte-d'Or, Ufaransa, 2 Mei 1806 - Enghien-les-Bains, Oise, 31 Desemba 1876) alikuwa mtawa wa Kanisa Katoliki katika shirika la Wavinsenti.

Mt. Katerina wakati wa kupata njozi (1830).

Alipata umaarufu kwa njozi alizosema alijaliwa na Bikira Maria kwamba alimkabidhi medali ya miujiza ili aieneze duniani kote.

Baada ya hapo alihudumia kwa upendo wazee na wagonjwa miaka 40.

Tarehe 28 Mei 1933 Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri na tarehe 27 Julai 1947 Papa Pius XII alimtangaza mtakatifu bikira.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Saint Catherine Labouré of the Miraculous Medal, by Joseph I Dirvin, CM, TAN Books and Publishers, Inc, 1958/84. ISBN|0-89555-242-6
  • Saint Catherine Labouré and the Miraculous Medal, Alma Power-Waters, Ignatius Press, San Francisco, 1962. ISBN|0-89870-765-X
  • The Life of Chatherine Labouré, by René Laurentin, Collins, 1980. ISBN|0-00-599747-X

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.