Kaunti ya Kiambu

Kaunti ya Kenya
Kuhusu mji, soma Kiambu

Kaunti ya Kiambu ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Kaunti ya Kiambu
Kaunti
Bonde la Ufa katika barabara kuu ya Nairobi-Nakuru, Lari
Bendera
Kiambu County in Kenya.svg
Kaunti ya Kiambu katika Kenya
Nchi Kenya
IlianzishwaMachi 4th 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Kati
Makao MakuuKiambu
GavanaFerdinand Waititu
Naibu wa GavanaDkt. James Nyoro
SenetaKimani Wamatangi
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Gathoni wa Muchomba
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Kiambu
SpikaStephen Ndichu[1]
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa60[2]
Maeneo bunge/Kaunti ndogo12
Eneo2,538.6 km2 (980.2 sq mi)
Idadi ya watu2,417,735
Wiani wa idadi ya watu952
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutikiambu.go.ke

Ilikuwa mojawapo ya wilaya za Kenya katika Mkoa wa Kati baada ya nchi kupata uhuru.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 2,417,735 katika eneo la km2 2,538.6, msongamano ukiwa hivyo wa watu 952 kwa kilometa mraba[3].

Kupakana na Nairobi kumeifanya iwe na idadi ya wakazi wengi mijini, kwa sababu ya maendeleo katika sekta ya mali yasiyohamishika. Sekta za viwanda na ukulima pia zimechangia kukuza kaunti hii kiuchumi.

Makao makuu ya kaunti hii ni mji wa Kiambu. Hata hivyo, utendaji wa kaunti hutekeleza majukumu yake kutoka Thika, ambayo wilaya yake imemezwa tena na Kiambu (2010).

Jiografia hariri

Kaunti hii imepakana na kaunti za Nairobi (kusini), Machakos (mashariki), Nakuru (magharibi), Nyandarua (kaskazini magharibi) na Murang'a (kaskazini).

Topografia ya kaunti ina nyanda za juu na nyanda za kati.

  1. Nyanda za juu kabisa zinapatikana katika kata ndogo ya Lari, ambazo ni kuenea kwa Safu za Nyandarua. Sehemu hiyo huwa na vilima vikali na ni chanzo cha maji.
  2. Nyanda za juu wastani ziko katika Limuru na sehemu za Gatundu Kusini, Gatundu Kaskazini, Githunguri na Kabete. Sehemu hizo zina vilima na tambarare zilizoinuka.
  3. Nyanda za kati hupatikana katika Juja, Thika na Ruiru. Sehemu hizo huwa kavu kidogo kuliko sehemu zingine za kaunti[4].

Kaunti ina vyanzo kadhaa vya maji.

Kiambu hupata misimu miwili ya mvua: Machi hadi Mei na Septemba hadi Disemba. Miezi kati ya Juni hadi Agosti huwa msimu wa baridi kali. Halijoto hutegemea na eneo. Maeneo ya nyanda za juu hupata baridi zaidi. Kata ndogo za Lari na Limuru na sehemu za magharibi za Gatundu Kusini, Gatundu Kaskazini na Githunguri hupata ukungu mzito na baridi ifikayo 7°c[4].

Serikali na Utawala hariri

Utendaji hariri

Gavana, sasa Ferdinand Waititu, ndiye mkuu wa kaunti na serikali. Yeye huchaguliwa kwa muhula wa miaka mitano katika uchaguzi mkuu. Ana nguvu za utendaji na za kuteua wanakamati wa Kamati ya Utendaji ya Kaunti baada ya kuidhinishwa na Bunge la Kaunti. Hata ingawa mji mkuu wa kaunti uko Kiambu, utendaji wa serikali uko mji wa Thika.

Bunge hariri

Bunge la Kaunti ya Kiambu ni la chumba kimoja. Lina wajumbe 60 waliochaguliwa kutoka wadi sitini za kaunti na wajumbe 27 walioteuliwa[5]. Kila mjumbe anashikilia hatamu ya miaka mitano, inayofanywa upya katika uchaguzi mkuu. Spika wa bunge na naibu wake huchaguliwa na wajumbe. Bunge la Kiambu liko katika mji wa Kiambu.

Mahakama hariri

Kuna Mahakama Kuu ya Kiambu iliyoanzishwa tarehe 20 Juni 2016. Ina jaji mmoja.[6]

Utawala hariri

Kamishna wa kaunti huteuliwa na Rais wa Kenya. Yeye ni mwakilishi wa rais kusaidia mambo ya utawala wa serikali ya kitaifa.

Kaunti ndogo hariri

Kaunti imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[7]:

Eneo bunge/kaunti ndogo Kata
Githunguri Githunguri, Githiga, Ikinu, Ngewa, Komothai 3
Kiambaa Cianda, Karuri, Ndenderu, Muchatha, Kihara
Kabete Gitaru, Muguga, Nyathuna, Kabete, Uthiru
Limuru Bibirioni, Limuru Kati, Ndeiya, Limuru Mashariki, Ngecha Tigoni
Lari Kinale, Kijabe, Nyanduma, Kamburu, Lari/Kirenga
Gatundu Kaskazini Gituamba, Githobokoni, Chania, Mang'u
Gatundu Kusini Kiamwangi, Kiganjo, Ndarugo, Ng'enda
Ruiru Githothua, Biashara, Gatongora, Kahawa Sukari, Kahawa Wendani, Kiuu, Mwiki, Mwihoko 1
Kikuyu Karai, Nachu, Sigona, Kikuyu, Kinoo
Juja Murera, Theta, Juja, Witeithie, Kalimoni
Thika Township, Kamenu, Hospital, Gatuanyaga
Kiambu Ting'ang'a, Ndumberi 3, Riabai, Township

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [8] hariri

  • Gatundu North 109,870
  • Gatundu South 122,103
  • Githunguri 165,232
  • Juja 300,948
  • Kabete 199,653
  • Kiambaa 236,400
  • Kiambu 145,903
  • Kikuyu 187,122
  • Lari 135,303
  • Limuru 159,314
  • Ruiru 371,111
  • Thika East 38,956
  • Thika West 245,820

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. http://www.nation.co.ke/counties/Kiambu/Stephen-Ndichu-Kiambu-Speaker/1183274-4087286-7a5c2kz/index.html
  2. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-12-03. Iliwekwa mnamo 2017-11-29.
  3. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  4. 4.0 4.1 4.2 COUNTY INTEGRATED DEVELOPMENT PLAN 2013 – 2017. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-06-19. Iliwekwa mnamo 2018-05-02.
  5. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-12-03. Iliwekwa mnamo 2017-11-29.
  6. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-10-11. Iliwekwa mnamo 2017-11-30.
  7. http://countytrak.infotrakresearch.com/Kiambu-county/
  8. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.