Kaunti ya Mombasa

Kaunti ya Kenya

Kaunti ya Mombasa imeshika nafasi ya wilaya ya Mombasa baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010. Kaunti hii ni mojawapo ya kaunti mbili ambazo pia ni jiji na ndio kaunti ndogo kabisa kati ya kaunti zote.

Kaunti ya Mombasa
Kaunti 001
Kaunti
Bendera Nembo ya Serikali
Utangamano kwa maendeleo
Mombasa County in Kenya.svg
Kaunti ya Mombasa katika Kenya
Coordinates: 4°03′S 39°40′E / 4.050°S 39.667°E / -4.050; 39.667
Nchi Kenya
Namba1
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Pwani
Makao MakuuMombasa
GavanaHassan Ali Joho
Naibu wa GavanaDkt. William Kingi
SenetaMohammed Faki
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Asha Hussein Mohammed
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Mombasa
SpikaArub Ibrahim Khatri
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa30
MahakamaMahakama ya Rufaa, Mombasa
Maeneo bunge/Kaunti ndogo6
Eneokm2 219.9 (sq mi 84.9)
Idadi ya watu1,208,333
Wiani wa idadi ya watu5,495
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutimombasa.go.ke

Inapakana na kaunti za Kwale na Kilifi ambazo pamoja na kaunti za Mombasa, Lamu, Tana River na Taita Taveta zilikuwa zinatengeneza Mkoa wa Pwani.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,208,333 katika eneo la km2 219.9, msongamano ukiwa hivyo wa 5,495 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu ya serikali ya kaunti yako katika jiji la Mombasa.

Jiografia hariri

Kaunti ya Mombasa inapakana na Bahari Hindi. Ina kisiwa cha Mvita ambacho huwa kati mwa Jiji la Mombasa. Kimetenganishwa na bara na Kijito cha Tudor na Kijito cha Port Reitz[2]. Vijito hivyo hugawanywa na Makupa Causeway. Maeneo hayo mengine ya bara yameunganishwa kwa feri na daraja. Ardhi yake ni tambarare.

 
Makupa Causeway; Kijito cha Tudor kushoto, Kijito cha Port Reitz kulia

Lindi la Bandari ya Kilindini, lenye kina cha mita 45-55, huiwezesha kuegeshwa meli kubwa[3].

Mombasa ina misitu asilia mitatu ambayo ni 6% ya misitu ya mikoko ya Kenya[4]. Misitu hiyo ni mojawapo ya makazi ya wanyamapori katika kaunti hii. Hata hivyo, uvunaji kupindukia wa miti, maeneo taka na kupanua ardhi baharini kumeharibu misitu hii na kuathiri wanyamapori wa majini na ardhini[5][6].

 
Bandari ya Mombasa, Kilindini

Kaunti ya Mombasa ina tabianchi ya tropiki[7]. Kwa kuwa iko kando na bahari, kiwango cha unyevuanga huwa juu. Hali ya hewa hutegemea pepo za monsuni. Kaunti hupata misimu miwili ya mvua: Aprili hadi Juni na Oktoba hadi Disemba.

Kubadilika kwa wastani wa hali ya hewa kumesababisha kiwango cha upwaji wa bahari kupanda na kuongezeka kwa halijoto, mambo ambayo yanatishia jiji la Mombasa na turathi ya Fort Jesus. Pia, mafuriko ya pwani, mmomonyoko katika fuko na kutoweka kwa mwamba tumbawe kumesababishwa na mabadiliko haya[8][9][5].

Uchumi hariri

Uchumi wa Mombasa na nchi ya Kenya kwa jumla hutegemea sana bandari ya Mombasa. Bandari ya Mombasa ndio bandari kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Bidhaa nyingi hupitia hapo kutoka na kuingia ndani ya nchi. Bandari hii pia hutegemewa na nchi ya Uganda, Burundi, Sudani Kusini, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda kupitisha bidhaa kama vile, mafuta[10].

 
Ufuko wa Nyali, Mombasa

Mombasa pia ni kituo kikuu cha utalii kwa sababu ya fuko zake zenye mchanga, Fort Jesus na Mji wa Kale. Baada ya mashambulizi kadhaa ya kigaidi katika miaka ya awali ya mwongo wa 2010 na Al Shabaab na vikundi vingine, utalii ulidorora[11][12]. Nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa pamoja na nchi zingine za magharibi zilianza kutoa tahadhari za safari. Baada ya Operesheni Linda Nchi, na juhudi za polisi kukumbana na ugaidi, juhudi zinaelekezwa kuimarisha utalii tena[13]. Pia, kuanzishwa kwa huduma ya reli mpya ya SGR kati ya Jiji la Mombasa na Nairobi, kumeongeza idadi ya watalii wa ndani[14].

Mnada wa Chai wa Mombasa ni mojawapo ya vituo vya unadi wa chai katika dunia. Mnada huu hunadi chai kutoka nchi za Kenya, Tanzania, Uganda Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi, Madagaska, Zambia na Zimbabwe. Kufikia mwaka wa 2017, ulikuwa soko ya pili kwa ukubwa ya uuzaji wa chai katika dunia[15].

Maeneo bunge hariri

Kaunti ya Mombasa ina maeneo bunge yafuatayo[16]:

Kaunti ndogo/Eneo bunge Kata
Changamwe Port Reitz, Kipevu, Airport, Changamwe, Chaani
Jomvu Jomvu Kuu, Miritini, Mikindani
Kisauni Mjambere, Junda, Bamburi, Mwakirunge, Mtopanga, Magogoni, Shanzu
Nyali Frere Town, Ziwa la Ngombe, Mkomani, Kongowea, Kadzandani
Likoni Mtongwe, Shika Adabu, Bofu, Likoni, Timbwani
Mvita Mji wa Kale/Makadara, Tudor, Tononoka, Majengo Ganjoni/Shimanzi

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019)[17] hariri

  • Changamwe 131,882
  • Jomvu 163,415
  • Kisauni 291,930
  • Likoni 250,358
  • Mvita 154,171
  • Nyali 216,57

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. www.knbs.or.ke
  2. Sant Bahadur Singh (1995). Emerging Frontiers of Urban Settlement Geography. M.D. Publications Pvt. Ltd. ku. 97–. ISBN 978-81-85880-83-9. 
  3. "Port of Mombasa, Kenya Archived 8 Julai 2018 at the Wayback Machine.". www.findaport.com. Shipping Guides Ltd. Retrieved 18 March 2018.
  4. "NATIONAL MANGROVE ECOSYSTEM MANAGEMENT PLAN" (PDF). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-17. Iliwekwa mnamo 2018-05-02. 
  5. 5.0 5.1 Atieno, Winnie. "Mombasa getting hotter as mangroves rapidly disappear from coastline - Business Daily". Iliwekwa mnamo 2018-05-02. 
  6. Mghenyi, Charles. "Waste, sea reclamation kill Mombasa mangroves, destroy forests". Iliwekwa mnamo 2018-05-02.  Text "The Star, Kenya" ignored (help)
  7. "CLIMATE: MOMBASA", Climate-Data.org, ilipatikana 13-04-2013
  8. Olingo, Allan. "East Africa’s coast is slowly sinking - The East African". Iliwekwa mnamo 2018-05-02. 
  9. Agutu, Nancy. "Climate doom: Rising seas, submerged hotels, thousands jobless". Iliwekwa mnamo 2018-05-02.  Text " The Star, Kenya " ignored (help)
  10. "History of The Port Of Mombasa", Halmashauri ya Bandari za Kenya, ilipatikana 13-04-2018
  11. "10 wajeruhiwa katika shambulio Kenya", BBC Kiswahili, ilipatikana 13-04-2018
  12. "GRENADE ATTACK KILLS ONE IN MOMBASA NIGHT CLUB Archived 2012-09-11 at Archive.today". The Star. 16 May 2012. Retrieved 31 May 2012.
  13. Charles Wasonga, "Serikali ikomeze utovu wa usalama kupiga jeki utalii", Taifa Leo, ilipatikana 13-04-2018
  14. Philip Mwakio, "Wildebeest migration and SGR boost tourism", The Standard, ilipatikana 13-04-2018
  15. GERALD ANDAE, "Mombasa tea sale records third best price globally", Business Daily, ilipatikana 13-04-2013
  16. http://countytrak.infotrakresearch.com/Mombasa-county/
  17. www.knbs.or.ke