Kawira Mwirichia

Msanii na mtunzaji kutoka Kenya aliyeishi Athi River

Kawira Mwiricha (1986 - 2020) [1] alikuwa msanii mwenye ujuzi mbalimbali, mtunzaji wa kazi za sanaa na mtetezi wa ushoga aliyeishi Athi River nchini Kenya. Ni msanii aliyefahamika kimataifa kwa kuchora kanga pamoja, uchoraji na uchongaji.

Maisha ya awali na elimu hariri

Kawira Mwiricha alipokea shahada yake ya uhandisi wa majengo kutoka Chuo kikuu cha Nairobi (Agosti 2007Desemba 2012).[2]

Kupitia Astraea Commslab, Mwirichia alisoma kozi ya mtandaoni ya uanaharakati wa ushoga. Mafunzo yake rasmi ya sanaa yalitoka kwa kozi za grafiki & uundaji wa mtandao katika Taasisi ya Teknolojia ya Juu pamoja na Taasisi ya Mafunzo ya Biashara ya Nairobi.

Alifariki nyumbani kwake na maiti yake ilikutwa tarehe 3 Novemba 2020 katika hali ya kuoza, ilhali aliripotiwa kupotea siku kadhaa kabla ya kukutwa[3].

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kawira Mwirichia kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.