Kiadyghe ni lugha ya Kikaukazi ya Kaskazini nchini Urusi, Uturuki, Yordani, Syria, Iraq na Israel inayozungumzwa na Waadyghe.

Mwaka wa 2010 idadi ya wasemaji wa Kiadyghe nchini Urusi imehesabiwa kuwa watu 117,500. Pia kuna wasemaji 316,000 nchini Uturuki (2014), 78,000 nchini Yordani (2013), 35,000 nchini Syria (2014), 34,000 nchini Iraq (2014) na 3,000 nchini Israel (2005).

Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiadyghe kiko katika kundi la Kikirkasi.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiadyghe kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.