Kibanda ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabanda kwenye visiwa vya Kei. Kwa asili Wabanda wametoka kisiwa cha Banda lakini lugha ya Kibanda imeachwa kuzungumzwa huko. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kibanda imehesabiwa kuwa watu 3000. Kwa vile Wabanda wengi wameanza kuacha lugha yao, Kibanda imekaribia kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibanda iko katika kundi la Kimaluku.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kibanda kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.