Kimanchu ni lugha ya Kitungusi nchini Uchina inayozungumzwa na Wamanchu. Ingawa idadi ya Wamanchu ni zaidi ya milioni kumi (kufuatana na sensa ya 2000), mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kimanchu imehesabiwa kuwa watu ishirini tu. Karibu Wamanchu wote huzungumza Kichina cha Mandarin, na lugha yao ya asili imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kimanchu kipo katika kundi la Kitungusi cha Kusini. Kimanchu huandikwa kwa alfabeti ya Kimongoli, na kuna fasihi andishi kwa karne kadhaa. Kimanchu kilikuwa lugha rasmi wakati wa nasaba ya Qing.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimanchu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.