Lugha ya Kimanksi (kwa lugha hiyo: Gaelg au Gailck; kwa Kiingereza: Manx) ni kati ya lugha za Kiselti, tawi la lugha za Kihindi-Kiulaya ambalo limerudi nyuma sana tangu zamani za Roma ya Kale lilipokuwa linatumika katika eneo kubwa sana la Ulaya hadi Uturuki wa leo.

Ramani inayonyesha lugha hizo zinapotumika hadi leo au zilipotumika katika karne za mwisho:      Ireland (Kieire)      Scotland (Kiskoti)      Isle of Man (Kimanksi)      Wales (Kiwelisi)      Cornwall (Kikornishi)      Brittany (Kibretoni)

Si lugha mama ya mtu yeyote tangu mwaka 1974, lakini kuna juhudi za kuifundisha katika kisiwa cha Man, kwa hiyo watu 2,000 hivi wanaijua[1].

Tanbihi hariri

  1. Crystal, David (2010). The Cambridge Encyclopedia of Language. Cambridge University Press. ISBN 978-0-521-73650-3.
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimanksi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.