Kiongota (pia Kibirale) ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Ethiopia inayozungumzwa na Waongota. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kiongota imehesabiwa kuwa watu kumi tu, maana yake lugha imekaribia kutoweka kabisa. Waongota wengi, ambao idadi yao ni 3400, wamebadili lugha kutumia Kitsamai badala ya lugha yao ya Kiongota. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiongota hakijaainishwa kikundi.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiongota kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.