Katika utarakilishi, kipembezo (pia: pembezo[1]; kwa Kiingereza: peripheral) ni kitumi chote cha tarakilishi ambacho kinatumika ili kuingia na kuondoa taarifa kutoka tarakilishi.

Vipembezo vya kutolea vinaitwa kiwambo na kipaza sauti.
Kipembezo cha kuingia kinaitwa baobonye

Kuna aina kadhaa za vipembezo.

  1. Kitumi cha kuingia ambacho kinatuma data tarakilishi, kama kipanya, baobonye, kamera pembuzi au kitambazo.
  2. Kitumi cha kutolea ambacho kinatoa kitoleo cha tarakilishi, kama kichapishi, skrini au kipaza sauti.

Tanbihi hariri

  1. "ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY (INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM.)". kamusi.kiswahilipedia.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-03-07. Iliwekwa mnamo 2020-11-24. 

Marejeo hariri

  • Kiputiputi, O. (2011). Kamusi sanifu ya kompyuta. Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, K.602.
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.