Kishazi tegemezi (alama yake ni: K/Teg) ni tungo ambayo inayotawaliwa na kitenzi kisichojitosheleza kimaana. Yaani, ni tungo ambayo hutawaliwa na kitenzi ambao hakitoi taarifa kamili. Kishazi tegemezi hutegemea msaada/lazima kiambatane na kishazi huru ndipo taarifa yake iweze kukamilika.

Mfano:

  • Mtoto anayecheza mpira / amevunjika mguu (mtoto anayecheza mpira = Kishazi tegemezi, amevunjika mguu = Kishazi huru).
  • Hotuba aliyoitoa Rais
  • Nyumba iliyojengwa bondeni
  • Wageni waliokuja jana
  • Ng'ombe aliyechinjwa
  • Ndizi zilizoiva

Sifa za kishazi tegemezi hariri

i/ Hakitoi taarifa kamili. Ili taarifa yake ikamilike ni lazima kiambatane na kishazi huru.

ii/Huundwa na urejeshi. Urejeshi huo hufanya kazi ya kutoa taarifa ya ziada kuhusu nomino.

iii/Si cha lazima sana katika tungo kwani kinaweza kuondolewa katika tungo na bado tungo hiyo ikabaki na maana kamili.

iv/Kinaweza ama kutanguliwa au kufuatiwa na kishazi huru.

Tazama pia hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kishazi tegemezi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.