Kislavoni cha Kusini

Kislavoni cha Kusini ni kundi la lugha za Kislavoni zinazozungumzwa kwenye Balkani (Ulaya ya Kusini-Mashariki).

Nchi ambako lugha ya Kislavoni cha Magharibi ni lugha rasmi;
Nchi ambako lugha ya Kislavoni cha Mashariki ni lugha rasmi;
Nchi ambako lugha ya Kislavoni cha Kusini ni lugha rasmi

Idadi ya wasemaji wa lugha hizi ni ni takriban milioni 34. Mwandiko hutumia alfabeti ya Kikyrili upande wa mashariki (Kibulgaria, Kiserbia, Kimasedonia) na alfabeti ya Kilatini upande wa magharibi (kama vile Kikroatia, Kislovenia). Kiserbokroatia kiliandkiwa kwa namna zote mbili.

Lugha hizi zimetengwa na eneo la wasemaji wengine wa Kislavoni kwa kanda lenye wasemaji wa Kijerumani (Austria), Kihungaria na Kiromania.