Klod (kwa Kifaransa Cloud; kwa Kilatini Clodoaldus) alikuwa padri kutoka ukoo wa kifalme wa Orleans huko Ufaransa (522 - 560 hivi)[1].

Sanamu ya Mt. Klod.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Septemba[2].

Maisha hariri

Bibi yake alikuwa mtakatifu Klotilda malkia.

Ndugu zake wawili waliuawa wakiwa bado watoto; yeye tu alinusurika kwa kukimbilia Provence[3] na kujinyima haki zote za kumrithi baba yake, mfalme Klodomer[4]. Pia aliwagawia fukara mali iliyombakia.

Baada ya kuishi kama mkaapweke chini ya Severini wa Paris, alipoona anatembelewa na wengi kwa ushauri kiasi kwamba hafaidiki na upweke akarudi Paris, alipopokewa kwa furaha.

Watu walimuomba askofu ampe upadrisho (551). Halafu alitoa huduma kwa muda fulani, kisha akarudi upwekeni, na hatimaye akaanzisha abasia karibu na Versailles[5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.