Koffi Olomide

Mwimbaji wa Kongo, mtunzi, mwigizaji na mtayarishaji

Antoine Koffi Olomidé (amezaliwa tarehe 13 Agosti 1956), ni mwimbaji, mtayarishaji, na mtunzi wa ngoma aina ya soukous kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Koffi Olomide

Alizaliwa Kisangani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mama mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na baba mzaliwa wa Kongo, na alilelewa katika mji wa Kinshasa.
Alienda Ufaransa kusoma. Akiwa Paris, alianza kucheza gitaa na kuandika nyimbo. Aliporudi Kongo, alikuwa mwanachama wa Viva la Musica, bendi ya Papa Wemba. Koffi aliimarisha mtindo wa polepole wa soukous, uliokuwa umeisha umaarufu. Aliuita mtindo huu Tcha Tcho, na ulipata umaarufu nje ya Kongo. Muziki wa Koffi unaweza kusababisha utata, maana hutumia matukio na mada inayofikiriwa vibaya na kihafidhina katika jamii. Yeye pia ameshiriki katika mradi wa muziki wa salsa wa Africando.

Koffi ameshinda tuzo nne za Kora katika Afrika ya Kusini na pia alishinda msanii bora katika Afrika ya Kati. Ameowa na ana watoto watano.

Albamu ya Olomide Haut de Gamme: Koweït, Rive Gauche imeorodheshwa katika Albamu 1001

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Koffi Olomide kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.