Koitalel Arap Samoei

Koitalel Arap Samoei alikuwa kiongozi shubavu wa Wanandi aliyeongoza vita vikali dhidi ya serikali ya upepari ya uingereza katika Africa Mashariki.Alikataa ujenzi wa reli iliyotekelezwa na wabeberu kwa sababu reli ilionekana kuwa mzingi kunyakua nchi ya yake ya Nandi.

Jumba la makumbusho la Koitalel Arap Samoei lilipo nandi nchini Kenya

Nafasi yake ilikuwa ya orkoiyot au mfalme. Kabla ya kufika kwa Waingereza Koitalel aliwahi kutabiri ya kwamba joka jeusi litemayo moto litafika Nandi na kuhatarisha maisha ya watu wake.

Reli ilipofika ikaonekana kama utimilifu wa utabiri wake.

Aliwaongoza Wanandi kupambana na Waingereza kwa miaka kumi na mbili. Captain Richard Meinertzhagen alifaulu kumwua 1905. Alimkaribisha Koitalel kwa majadiliano ya kumaliza vita. Badala ya kuongea naye akamwua moja kwa moja pamoja mawaziri wake 23.

Baada ya kukosa kiongozi,Wanandi walishindwa kupigana na Captain Richard na ujenzi wa reli ukaendelea.