Konstantinopoli (kwa Kigiriki: Κωνσταντινούπολις - Konstantinupolis, yaani "mji wa Konstantino") ni mji ulioanzishwa na Wagiriki wa kale kwa jina la Bizanti mnamo 660 KK ukapewa na Kaisari Konstantino jina lake mwenyewe na kufanywa mji mkuu wa Dola la Roma kuanzia mwaka 330 BK.

Konstantinopoli ya kale (nyekundu) pamoja na miji yake ya kando (kijani) ndani ya eneo la Istanbul ya leo

Baadaye ukabaki mji mkuu wa Dola la Roma la Mashariki au milki ya Bizanti kati ya 395 hadi 1453.

Baada ya kutwaliwa na Waturuki Waosmani ulikuwa mji mkuu wa milki ya Osmani hadi 1922.

Mji ulianzishwa upande wa Ulaya wa mlangobahari wa Bosporus kati ya hori ya "pembe ya dhahabu" na Bahari ya Marmara.

Leo hii mji huo wa Kituruki umevuka Bosporus ukienea hata upande wa Asia.

Ulibadilishiwa jina mara kadhaa katika historia yake ndefu: Bizanti, Roma Mpya (kwa Kigiriki: Νέα Ῥώμη), Konstantinopoli, tena Bizanti, Stambul, halafu Istanbul (tangu mwaka 1930).

Katika Ukristo ni muhimu kama makao ya Askofu wa pili kwa heshima kati ya Maaskofu wote duniani, kadiri ya orodha iliyotolewa na mitaguso mikuu ya karne ya 4.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Konstantinopoli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.