Kordilera ya Amerika

Kordilera ya Amerika ni mlolongo wa safu za milima kunjamano unaopita katika Amerika Kaskazini hadi Amerika Kusini upande wa magharibi kufuatana na pwani ya Bahari Pasifiki. Unaendelea hadi Antaktiki ya magharibi.[1] Kordilera ("cordillera") ni jina la Kihispania inayomaanisha safu ya milima.

Rangi ya kahawia inaonyesha safu za milima ya Kordilera ya Amerika inayofuatana na pwani la Pasifiki katika Amerika Kaskazini na Kusini
Safu ya Andes, Amerika Kusini

Kaskazini mfumo huo wa milima unaanzia Alaska kaskazini hadi kusini, mlolongo huu wa mwingiliano unaoingiliana na safu sambamba huanza huko Alaska unapita Yukon na British Columbia na kuendelea katika safu za Rocky Mountains.

Huko Mexico milima ya kordilera inaendelea kupitia Sierra Madre ya Mashariki na Sierra Madre ya Mashariki, pamoja na milima ya rasi ya Baja California.

Kusini mwa Meksiko milima ya kordilera inaendelea katika Amerika ya Kati, yaani huko Guatemala, Honduras, Nicaragua, Costa Rica na Panama.

Kuanzia huko inaendelea upande wa kusini kama Milima ya Andes ya Amerika Kusini.

Katika nchi za Kolombia, Venezuela, Ekuador, Peru, Bolivia, Argentina, na Chile Andes inaendelea kama mfumo wa safu zinazoenea kandokando hadi ncha ya Amerika Kusini huko Tierra del Fuego.

Mfumo huo unaendelea chini ya bahari ya Kusini hadi kuonekana tena kwenye milima ya Grahamland kwenye Rasi ya Antaktiki.

Tanbihi hariri

  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.