Kosta Rika (kwa Kihispania: Costa Rica, yaani Pwani Tajiri) ni nchi ya Amerika ya Kati.

Kosta Rika
Ramani ya Kosta Rika.

Imepakana na Nikaragua na Panama; kuna pwani ya Pasifiki upande wa magharibi na pwani ya Bahari ya Karibi upande wa mashariki.

Kosta Rika ilikuwa nchi ya kwanza duniani ya kufuta jeshi lake kikatiba. Pia inaongoza kwa kuhifadhi mazingira.

Mji mkuu ni San José.

Historia hariri

Kabla ya kufika kwa Wahispania katika karne ya 16, nchi ilikaliwa na Waindio wachache.

Mwaka 1821 koloni hilo lilijiunga na ghasia ya maeneo mengine ya Amerika ya Kati dhidi ya utawala wa Hispania.

Mwanzoni nchi hizo ndogo zilijiunga na Meksiko lakini baada ya miaka miwili zilianzisha "Shirikisho la Amerika ya Kati" lililokwisha mwaka 1839.

Tangu mwaka 1847 Kosta Rika imekuwa nchi ya kujitegemea kabisa.

Mwaka 1948 kulitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo viliwahi kwisha. Mwaka uliofuata nchi ilifuta kabisa jeshi hadi leo[1][2][3].

Watu hariri

Wakazi wengi (65.8%) wana asili ya Ulaya, mbali ya machotara Wazungu-Waindio (13.65%) na wahamiaji wenye asili yoyote (9.03%). Waindio, ambao ndio wakazi asili, ni 2.4% tu.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania.

Upande va dini, walio wengi ni wafuasi wa Yesu katika Kanisa Katoliki (70.5%: ndiyo dini rasmi) au madhehebu ya Uprotestanti (13.08%). Nje ya Ukristo, unaongoza Ubuddha (2.3%).

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. El Espíritu del 48. Abolición del Ejército (es).
  2. Costa Rica. World Desk Reference. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-02-11. Iliwekwa mnamo 2021-04-02.
  3. Costa Rica. Uppsala University. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-05-10. Iliwekwa mnamo 2021-04-02.

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kosta Rika kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.