Kristo Mfalme ni sifa mojawapo ya Yesu katika imani ya Ukristo.

Kioo cha rangi cha Kanisa Kuu la Wamelkiti huko Roslindale, Massachusetts, kikimuonyesha Kristo amevaa kama Kaisari wa Bizanti.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Jesus
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Inahusiana na wazo la Ufalme wa Mungu ambapo Kristo anachorwa kuwa ametawazwa upande wa kuume wa Mungu kama mshiriki wa mamlaka yake juu ya wote na vyote[1]

Katika Biblia hariri

Maneno "Kristo" na "mfalme" hayatumiwi pamoja katika Injili, kwa kuwa tayari "Kristo" ni jina la kifalme likimaanisha "Mpakwamafuta".

Humo Kristo anaitwa wazi mfalme (βασιλεύς) mara kadhaa, [2]

Pia Waraka wa kwanza kwa Timotheo (6:14–15) unatumia kwa Yesu maneno ya Kumbukumbu la Torati 10:17: "mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana" (Βασιλεὺς βασιλέων καὶ κύριος κυρίων).

Zaidi ya yote, Yesu mwenyewe alijiita mfalme na kujitambulisha hivyo akieleza atakavyoendesha hukumu ya mwisho (Math 25).

Teolojia hariri

Ukristo unafundisha kuwa siku arubaini baada ya kufufuka, Yesu alipaa mbinguni mbele ya wanafunzi wake. Hataonekana tena rasmi mpaka arudi siku ya mwisho. “Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni” (Mdo 1:11). “Mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu” (Kol 3:1).

Wakristo wanahusika na kupaa kwake, kwa sababu yeye ni kichwa chetu nao ni viungo vya mwili wake: hivyo amewatangulia kwa Baba awaombee Roho Mtakatifu wakafike kwake. Mwenyewe ameahidi, “Mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo” (Yoh 14:3). “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea” (Rom 8:33-34). “Yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee” (Eb 7:24-25).

Hivyo, utawala wa Yesu umeshaanza nao utakamilika atakaporudi kuwahukumu wazima na wafu kwa kutenganisha moja kwa moja wema na wabaya. “Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti” (1Kor 15:25-26). Hapo katikati “watafanya vita na Mwanakondoo, na Mwanakondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme” (Ufu 17:14).

Utawala wa Yesu umeanza hasa katika Kanisa lake linalokusanya wale waliomuamini kuwa ni Bwana wakaokolewa. Mungu “alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake” (Kol 1:13). Yesu alisema, “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu… Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu” (Yoh 18:36,37). “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza” (Lk 17:20). “Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia” (Math 13:33). Baada ya kufufuka, aliwajibu Mitume waliomuuliza kuhusu wakati wa kurudisha ufalme: “Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” (Mdo 1:7-8).

Sikukuu ya Kristo Mfalme hariri

Katika Kanisa Katoliki sikukuu hiyo ilianzishwa na Papa Pius XI mwaka 1925, na inaadhimishwa Jumapili ya mwisho ya Mwaka wa Kanisa, kama kilele chake.

Hata baadhi ya madhehebu ya Uprotestanti wanaiadhimishwa karibu na mwisho wa mwaka wa liturujia.

Tanbihi hariri

  1. Philip Edgecumbe Hughes A Commentary on the Epistle to the Hebrews p401 1988 "The theme of Christ's heavenly session, announced here by the statement he sat down at the right hand of God, .. Hebrews 8:1 "we have such a high priest, one who is seated at the right hand of the throne of the Majesty in heaven")"
  2. So in Matthew 2:2 ("Where is the newborn king of the Jews?"). In John 18, Pilate refers to the implication that the Christ is a royal title by inquiring explicitly if Jesus claims to be the "king of the Jews" (βασιλεὺς τῶν Ἰουδαίων). Similarly, in John 1:49, a follower addresses Jesus as "the king of Israel" (ὁ βασιλεὺς τοῦ Ἰσραήλ).

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kristo Mfalme kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.