Kundi la majarra

(Elekezwa kutoka Kundi la galaksi)

Kundi la majarra (kwa Kiingereza: galaxy group) ni idadi ya majarra zinazoshikamana katika anga-nje. Maana zinaathiriana kwa njia ya mvutano wake. Katika mpangilio huo ni hadi majarra 50 zinazotazamwa kuwa kundi.

Kundi la majarra HCG 16, ilivyoonekana kwa darubini ya Hubble

Kama idadi ya majarra zinazoshikamana ni kubwa zaidi jumla yake ni fundo la majarra.

Majarra za kundi moja zinaenea katika nafasi yenye kipenyo cha takriban miakanuru milioni 10 hivi; masi ya majarra zote kwa pamoja ndani ya kundi ni hadi masi za Jua 1013.[1]

Majarra yetu ya Njia Nyeupe ni sehemu ya kundi janibu la majarra pamoja na majarra 40 hivi nyingine.[2] Pamoja na Njia Nyeupe kuna Majarra ya Mara (inaitwa pia M31) katika kundinyota Mara, ya M33 katika Pembetatu na majarra ndogo kama Mawingu ya Magellan.

Marejeo

  1. UTK Physics Dept. "Groups of Galaxies". University of Tennessee, Knoville. Iliwekwa mnamo September 27, 2012.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. Mike Irwin. "The Local Group". Iliwekwa mnamo 2009-11-07. 
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kundi la majarra kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.