Kyebitembe ni kata ya Wilaya ya Muleba katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35529 [1].

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 25,460 waishio humo.[2]

Kata hii imepakana na ziwa Burigi. Pia hifadhi ya Mbuga ya Wanyama ya Burigi inapatikana ndani ya kata hii.

Ni mwendo wa saa 3.5 kwa usafiri wa Hiace kutoka kata ya Kyebitembe mpaka stendi ya mkoa iliyo ndani ya Manispaa ya mji wa Bukoba.

Pia ndani ya kata hii kuna sekondari moja ambayo ni Shule ya Sekondari Kanyeranyere na shule 8 za msingi ambazo ni Nyamilanda, Kanyeranyere, Kabungo, Kyebitembe, Kyabishagao, Nyanjubi, Kagasha na Kasindaga.

Marejeo hariri

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. Sensa ya 2012, Kagera - Muleba-District-Council
  Kata za Wilaya ya Muleba - Mkoa wa Kagera - Tanzania
 

Biirabo | Bisheke | Buganguzi | Buhangaza | Bulyakashaju | Bumbire | Bureza | Burungura | Goziba | Gwanseli | Ibuga | Ijumbi | Ikondo | Ikuza | Izigo | Kabirizi | Kagoma | Kamachumu | Karambi | Kasharunga | Kashasha | Katoke | Kerebe | Kibanga | Kikuku | Kimwani | Kishanda | Kyebitembe | Mafumbo | Magata Karutanga | Mayondwe | Mazinga | Mubunda | Muhutwe | Muleba | Mushabago | Ngenge | Nshamba | Nyakabango | Nyakatanga | Ruhanga | Rulanda | Rutoro


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kyebitembe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.