Lemuri-spoti
Lemuri-spoti wa Randrianasolo
Lemuri-spoti wa Randrianasolo
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota (Viumbe walio na seli zenye kiini)
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
Nusuoda: Strepsirrhini (Wanyama wanaofanana zaidi na lemuri)
Oda ya chini: Lemuriformes (Wanyama kama kima)
Familia ya juu: Lemuroidea (Lemuri)
Familia: Lepilemuridae (Lemuri walio na mnasaba na Lemuri mkia-miviringo)
Jenasi: Lepilemur
I. Geoffroy, 1851
Ngazi za chini

Spishi 26:

Lemuri-spoti (kutoka Kiingereza: sportive lemur) ni spishi za lemuri wa jenasi Lepilemur, jenasi pekee ya familia Lepilemuridae. Kama lemuri wote wanatokea Madagaska tu. Lemuri hawa ni wakubwa kiasi na wana manyoya kahawiakijivu kuelekea mekundu mgongoni na meupenjano chini. Urefu wa mwili wao ni sm 30-35 na mkia una urefu sawa. Uzito wao ni hadi g 900. Wana safu ya seli kama kioo (tapetum lucidum) mbele ya retina inayoakisi mwanga, kwa hivyo macho yao yana mng'ao (eyeshine). Hula majani hasa.

Spishi hariri

Picha hariri

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.