Leonsi wa Bordeaux

Leonsi wa Bordeaux (alifariki Bordeaux, Ufaransa, kabla ya 574 akiwa na miaka 54) alikuwa askofu wa kumi na tatu mji huo[1].

Habari chache za maisha yake zimo katika Historia Francorum ya Gregori wa Tours na katika Carmina ya Venansi Fortunati.[2]

Aliwahi kwenda vitani Hispania na kuoa.

Baada ya kupata uaskofu alishiriki mitaguso kadhaa akauitisha mmoja huko Saintes.[3]

Pia anakumbukwa kwa misaada aliyowapa maskini na kwa ujenzi wa makanisa mbalimbali[4].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Julai[5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/61720
  2. Fisquet, La France pontificale… Bordeaux, p. 39.
  3. Monumenta Germaniae Historica, Concilia aevi Merovingici Archived 4 Septemba 2019 at the Wayback Machine., Legum, Sectio III, Concilia, Tomus I, Hannoverae 1893, p. 112, r. 6; p. 117, r. 12; p. 120, r. 29; p. 145, r. 22.
  4. Viard, Bibliotheca Sanctorum, vol. VII, col. 1322.
  5. Martyrologium Romanum

Marejeo hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.