Louis Braille (Coupvray, 4 Januari 1809 - 6 Januari 1852) alikuwa mvumbuzi wa Ufaransa aliyebuni alfabeti ya Braille, ambayo huwasaidia watu wasioona kusoma. Braille husomwa na vipofu kwa kupitisha vidole juu ya karatasi.

Louis Braille
Louis Braille

Alichomwa kwa bahati mbaya na msharasi kwenye jicho lake moja wakati akiwa kwenye duka la baba yake. Kwa kipindi hicho kulikuwa hakuna antibaotiki na jicho lake liliathirika. Ambukizo hilo lilisambaa kwenye jicho lake lingine na mwishowe akawa ameathirika macho yote mawili, hivyo kuwa kipofu.

Braille alikufa huko Paris akiwa na umri wa miaka 43 kwa kupatwa na kifua kikuu.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Louis Braille kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.