Lugha za Kibalti (pia: Kibaltiki) ni kundi la lugha za Ulaya ambazo ni tawi la familia ya lugha za Kihindi-Ulaya.

Makabila ya Wabalti takriban miaka 800 yaliyopita.

Wasemaji wao wanapatikana katika maeneo upande wa mashariki-kusini ya Bahari Baltiki. Leo hii kuna lugha 2 za Kibalti ambazo ni Kilithuania na Kilatvia.

Zamani kulikuwa na lugha zaidi lakini hizi zilikwisha hadi karne ya 18. Makabila yaliyotumia lugha hizi ziliwahi kukalia maeneo kati ya mto Vistula na milima ya Urali. Tangu mnamo mwaka 1200 BK yalifikia chini ya utawala wa milki za Waslavoni (Poland, Urusi) au Wajerumani na wasemaji wengi walibadilisha lugha walipokea lugha za Kislavoni au za Kigermanik.

Lugha za ibalti ni maarufu kwa sababu sarufi yao imebaki karibu sana kwa Kihindi-Kiulaya asilia kuliko lugha zote nyingine zilizopo leo hii. Uhusiano huu unaonekana kwa kulinganisha lugha ya Veda ya Uhindi na lugha za Kibalti.