Lugha za Kihindi-Kiajemi

Lugha za Kihindi-Kiajemi ni kundi kubwa zaidi katika familia ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Zinajumuisha lugha za Kihindi-Kiarya na lugha za Kiajemi (Irani). Zinazungumzwa zaidi kwenye Bara Hindi na Nyanda za Juu za Iran. Hapo zamani zilitumiwa pia katika Asia ya Kati, mashariki mwa Bahari ya Kaspi .

Lugha za Kihindi-Kiulaya; buluu: maeneo ya lugha za Kihindi-Kiajemi

Lugha za Kihindi-Kiarya hariri

Kuna karibu lugha 221 za Kihindi-Kiarya (Indic), zenye jumla ya wasemaji zaidi ya milioni 800.

Lugha za Kiajemi (Kiirani) hariri

Kuna karibu lugha 86 za Kiajemi, zenye wasemaji kati ya milioni 150 hadi 200.

Kinuristani, Kibangani, na Kibadeshi hariri

Wasomi wengine huchukulia lugha za Kinuristani na Kibangani kama sehemu ya kikundi kidogo cha Kihindi-Kiarya, lakini wengine wanazichukulia kama vikundi viwili tofauti vya Kihindi-Kiajemi. Lugha ya Kibadeshi pia ni lugha ya Kihindi-Kiajemi isiyopangwa bado kimakundi.

Vyanzo hariri