Magindu ni kata ya Wilaya ya Kibaha Vijijini katika Mkoa wa Pwani, Tanzania, yenye postikodi namba 61211 .

Kata ya Magindu
Nchi Tanzania
Mkoa Pwani
Wilaya Wilaya ya Kibaha Vijijini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 6,785

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 6,785 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,991 [2] walioishi humo.

Magindu imepakana na Wilaya ya Morogoro vijijini kwa upande wa kusini na magharibi, kata ya kwala kwa upande wa mashariki na Mji wa Chalinze kwa upande wa kaskazini. Kijiji cha Magindu kilitokana na neno la Kikwele "ng'indu" lenye maana ya kima kwa Kiswahili waliopatikana kipindi cha ujenzi wa reli ya kati toka Dar kwenda Kigoma iliyopitia kijiji hapo.

Wakazi wa kijiji na kata ya Magindu ni mchanganyiko wa Wakwele na Wamaasai hususani vijiji vya Gumba, Gwata na Magindu pia wakutu wanaopatikana kijiji cha Lukenge. Kijiji cha Magindu ni moja ya vijiji vichache vilivyojariwa rasilimali watu, misitu na ardhi ya rutuba. Wanakijiji wa Magindu kama ilivyo vijiji vingine Tanzania wana mila na desturi za kabila lao la Wakwele na hucheza ngoma za jando kwa wavulana na uny'ago kwa wasichana ambazo mara nyingi hufanyika kipindi cha mavuno au mlao kama inavyojulikana huko.

Magindu ni kijiji ambacho pia kimejaliwa kupata huduma muhimu za kijamii kama shule ya msingi na sekondari, kituo cha afya na barabara yenye kiwango cha kokoto inayounganisha Magindu na Chalinze ya wilaya ya Bagamoyo ila bado kuna tatizo la umeme ambao serikali imeanza mipango ya kupeleka umeme huko. Vitongoji vya Magindu ni Mizuguni ambacho ni kijiji kipya, Magindu mjini, Lukarasi, Mnyonge na Kuyu.

Shughuli kuu ya kipato kwa wananchi wa magindu ni kilimo na biashara ndogondogo zinazofanyika eneo la magengeni lililopo Magindu mjini pia vijana hujishughulisha na uchomaji wa mkaa ili kujipatia kipato.

Matatizo mengine yanayoikabili kata ya Magindu ni migogoro ya wakulima na Wamaasai ambalo ni tatizo kwa muda mrefu bila kupata ufumbuzi wa kudumu.

Marejeo

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. Sensa ya 2012, Pwani - Kibaha DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-06-10.
  Kata za Wilaya ya Kibaha Vijijini - Mkoa wa Pwani - Tanzania  

Bokomnemela | Dutumi | Gwata | Janga | Kawawa | Kikongo | Kilangalanga | Kwala | Magindu | Mlandizi | Mtambani | Mtongani | Ruvu | Soga


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Magindu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.