Majimbo ya Rio de la Plata

Majimbo ya Rio Plata yalikuwa dola tangulizi la nchi za kisasa za Argentina, Bolivia, Paraguay na Uruguay. Maeneo yake yaliwahi kuunganishwa katika ufalme mdogo au jimbo kuu la La Plata ndani ya milki ya Hispania, lenye mji mkuu katika Buenos Aires.

Majimbo ya Rio de la Plata

Jina limetokana na mto Rio de la Plata ambao ni mto mkuu wa Amerika Kusini upande wa kusini wa mto Amazonas.

Historia hariri

Kuanzia mwaka 1810, baada ya uvamizi wa Ufaransa katika Hispania na kujiuzulu kwa mfalme, harakati za kutafuta uhuru zilianza katika makoloni ya Hispania huko Amerika Kusini. Mfalme mdogo (au gavana mkuu) wa Rio Plata alifukuzwa na serikali mpya iliundwa iliyokuwa na wawakilishi kutoka Buenos Aires pekee. Serikali hiyo ilitangaza mwanzoni kwamba ilitaka kumtambua mfalme aliyelazimishwa na Ufaransa kujiuzulu, lakini ilianza pia kujenga dola jipya.

Majimbo ndani ya umoja huo yalifuata mielekeo tofauti na matokeo yake yalikuwa mfululizo wa mafarakano na vita kati ya maeneo yake, hasa kwa sababu majimbo ya mbali hayakuwa tayari kufuata maazimio ya Buenos Aires.

Paragua tayari mwaka 1811, Uruguay ilifuata mwaka 1815. Maeneo ya Bolivia yaliendelea kutawaliwa na jeshi la Hispania kutoka Peru hadi kupata uhuru wake mnamo 1825.

Halmashauri ya Buenos Aires ilitangaza hatimaye uhuru wa Majimbo ya Rio Plata kwenye mwaka 1816. Jina rasmi kwa Kihispania lilikuwa Provincias Unidas del Rio de la Plata yaani Umoja wa Majimbo ya Rio de la Plata; kwa muda mfupi yalitumia pia jina la Provincias Unidas de Sudamerica yaani Umoja wa Majimbo ya Amerika Kusini.

Lakini Paraguay, Uruguay na Bolivia yote ziliondoka katika umoja wa jimbo la awali la Hispania. Hivyo ni Argentina pekee iliyobaki ikiendelea kutumia jina la "Umoja wa Majimbo ya Rio Plata" kama jina rasmi katika katiba yake, pamoja na jina la "Taifa la Argentina" (Nación Argentina).[1]

Kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka kadhaa, majimbo yafuatayo yalijiunga na kuunda

Marejeo hariri

  1. The Constitution: "Art. 35. – Las denominaciones adoptadas sucesivamente desde 1810 hasta el presente, a saber: Provincias Unidas del Río de la Plata; República Argentina, Confederación Argentina, serán en adelante nombres oficiales indistintamente para la designación del Gobierno y territorio de las provincias, empleándose las palabras 'Nación Argentina' en la formación y sanción de las leyes." ("Article 35. The denominations successively adopted from 1810 to the present – United Provinces of the Río de la Plata and Argentine Republic, Argentine Confederation – shall henceforth be interchangeable official names to describe the Government and territory of the provinces. The phrase 'Argentine Nation' is used for the formulation and the enactment of laws.")