Majira ya kupukutika majani

msimu unaofuata baada ya majira ya joto na msimu kabla ya msimu wa baridi
(Elekezwa kutoka Majira ya kupuputika majani)

Majira ya kupukutika majani (kwa Kiingereza Fall au Autumn)[1] ni mojawapo kati ya majira manne ya kanda za wastani, na halijoto yake ni ya baridi kiasi. Kadiri ya umbali na ikweta, mchana unazidi kuwa mfupi na usiku kuwa mrefu.

Uzuri wa majani kupuputika katika Green Mountain National Forest.

Pamoja na hayo, miti mingi, isipokuwa misonobari na misanduku, inaweza ikapotewa na majani yote: ndiyo asili ya jina la majira.

Kwa Kiswahili majira ya namna hiyo pia huitwa masika.

Yanafuata majira ya joto (kwa Kiingereza "Summer") na kutangulia majira ya baridi (kwa Kiingereza "Winter").

Majira hayo yanatokea duniani kwa nyakati tofauti kadiri eneo husika lilivyo kaskazini au kusini kwa ikweta. Hata katika nchi ileile, kwa mfano Kenya, majira ni tofauti upande huu na upande huu wa ikweta.

Tanbihi hariri

  1. "Oxford Dictionary on the North American usage of Fall". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-30. Iliwekwa mnamo 2015-04-04. 

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Majira ya kupukutika majani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.